HEINEKEN BEVERAGE IMEINGIA UBIA NA KAMPUNI YA KITANZANIA MABIBO BIA KWA AJILI YA USAMBAZAJI
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya Heineken Beverage imeingia makubaliano na
kampuni ya kitanzania Mabibo bia kwa ajili ya usambazaji wa bia ya Windhoek inayotengenezwa nchini Namibia.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo julai 31,2024 Meneja Mkazi wa Kampuni ya Heineken Obabiyi Fagade amesema lengo la kuingia ushirikiano huo ni mkakati mahususi wa kusaidia biashara za ndani na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania na kupata fursa za ukuaji katika ya kusini mwa Afrika
"Ushirikiano huo na Mabibo bia ,wines na spirits ni kufungua ukurasa mpya kwa kuunganisha utaaalamu wetu wa Kimataifa Kama Heineken na ujuzi mkubwa walionao katika soko la ndani,tuna uhakika katika uwezo wetu wa kuwasilisha bidhaaa na huduma za kipekeee kwa watej wetu Tanzania";,amesema .
Ameongeza kuwa Heineken imedhamiria kutoa huduma za kipekeee kupitia vinywaji vyenje ubora wa hali ya juu ambavyo vinakizi ladha ya watumiaji.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Bia Jerome Rugilamalila amesema mkataba huo wa kibiashara umekuja baada ya kampuni ya Mabibo na Namibia Breweries kukubalina kuvunja mkataba walioingia mwak 2008.
Comments
Post a Comment