KAMPUNI YA ORYX GESI TANZANIA YAFANYA KUFURU KWA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI ,WAGAWA MITUNGI YA GESI NA MAJIKO YAKE.
![Image](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEidvYKspARZ9aAdWKJImpc_ec5DZko6uzutdBYM9hBCpky6dR-K2mAsSu03tb27QvtNJu_pDARm0H2l6sypLoMkYLiyh7Op5XeiPRvqsSJSsb-QEWj5GzbpA1HKCxomoTxh5cX41FYTudM/s1600/IMG_ORG_1714493141560.jpeg)
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM KAMPUNI ya Oryx Gesi imekabidhi mitungi ya gesi ya kilo 15 na majiko yake Kwa wahariri ,waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya Mpango wake wa kuhamasisha matumisi ya Nishati safi ya Kupikia Kwa watanzania Akizungumza katika hafla fupi ya ugawaji wa mitungi hiyo iliyofanyika Leo April 30 ,2024 Kwenye Kiwanda cha Kampuni kilichopo wilayani kigamboni jijini Dar es salaam mkurugenzi mkuu BenoIte Araman Oryx Gas Tanzania wanauwezo wa kusambaza na kutoa Gas Tanzania bara na visiwani kwa wakati, muda wowote na sehem zote. "Kwetu Oryx Gesi tukio hili tumelipa uzito mkubwa na hii inatokana na umuhimu wenu katika jamii yetu, kwetu sisi Oryx vyombo vya habari vimekuwa daraja na kiunganishi kikubwa cha kufikisha taarifa zinazohusiana na nishati safi ya kupikia na hasa inayotokana na gesi ya oryx kwa jamii."Amesema mkurugenzi Araman Nakuongeza kuwa "Sote tunafahamu Serikali yetu ya Awamu ya Sit...