JENERALI MABEYO AWAVISHA VYEO MAKAMISHNA WAPYA NGORONGORO
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu) Aprili,29, 2024 amewavisha vyeo maafisa Uhifadhi wakuu waliopandishwa vyeo hivi karibuni katika tukio lililofanyika ofisi za Makao makuu ya NCAA Karatu Mkoani Arusha.
Waliovishwa vyeo ni Afisa Uhifadhi Mkuu Lilian Magoma ambaye amepandishwa na kuvishwa cheo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia idara ya Mipango, tathmini na ufuatiliaji na Afisa Uhifadhi Mwandamizi wa Rasilimali watu Salma Chisonga aliyepandishwa cheo amevishwa cheo kuwa Kamishna msaidizi Mwandamizi wa uhifadhi, Rasilimali watu na Utawala.
Jenerali Mabeyo amewataka makamishna wapya kufanya kazi kwa kujituma na kuzingatia viapo vyao katika misingi ya uzalendo, maadili ya utumishi, ushirikiano, maarifa na bidii ya kazi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Comments
Post a Comment