ULEGA AHIMIZA UWEKEZAJI WA MITAJI SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI




Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega  amesema sekta za mifugo na uvuvi zinaweza kuwa na tija kubwa zaidi kama taasisi za kifedha zitaendelea kuwekeza mitaji katika shughuli za mifugo na uvuvi ili ziweze kuzalisha kwa tija na hivyo kuchangia vyema kwenye pato la taifa.

Ulega amesema hayo wakati akifafanua baadhi ya hoja za wadau wa Kongamano la Uwekezaji la CRDB lililopewa jina la “Uwekezaji Day 2024”linalofanyika jijini Dar es Salaam leo 2024. 

Amesema sekta za mifugo na uvuvi zinaweza kuwa na  tija kubwa katika uchumi wa taifa hivyo
ni muhimu taasisi za kifedha ikiwemo CRDB kuendelea kuwekeza mitaji ili kuinua wadau wanaojishughulisha na sekta hizo.

“Nawapongeza CRDB kwa kuaandaa Kongamano hili kubwa la uwekezaji day, ombi langu kwenu, jukwaa hili liwe chachu ya kubadili sekta hizi za uzalishaji kwa kuongeza mitaji ili kuchechemua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla”, amesema

Akizungumza katika mahojiano maalumu ambayo yamefanyika kwenye kongamano la uwekezaji Mtendaji Mkuu wa LSSL Edmond Matafu amesema kuwa wanayo teknolojia ya kisasa ya kupima udongo ambayo inamrahisishia mkulima kutambua aina ya udongo



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025