JENISTA MHAGAMA NYOTA ILIYOZIMIKA GHAFLA.

   Timothy Marko, DmNewsnline

               
Jenister Mhagama ni Mwanasiasa maarufu kutoka Tanzania ambaye amehudumu kwa miaka mingi katika uongozi wa Serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

Marehemu Mhagama alizaliwa Juni 23, 1967 katika Wilaya ya Songea Mjini, Mkoani Ruvuma Nchini Tanzania.

 Jenister Alipata Diploma ya Ualimu kutoka chuo Cha ualimu wilaya ya  Korogwe (Teachers Training College)mkoani Tanga na aliwahi kufanya kazi kama mwalimu kabla ya kuingia kwenye siasa. 

Jenista Mhagama  kifo chake kimetokea leo Desember 11,2025 akiwa bado ni mmoja wa viongozi wakubwa wa taifa, na taarifa ya kifo chake ili tangazwa rasmi na Bunge na vyombo vya habari nchini Tanzania

Jenista Mhagama alikuwa Mbunge na kiongozi ndani ya Serikali kabla ya awamu hii alikuwa wa afya wa Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Pia marehemu Jenister alikuwa mstari wa mbele katika masuala ya sera, afya, ajira, vijana na uongozi wa umma na  alijulikana kwa huduma yake ya umma na mchango wake kwa maendeleo ya sekta mbalimbali nchini Tanzania. 
 
      Uchagizaji wa Uongozi: 

Jenister alikuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma tangu 2005 hadi wakati wa kifo chake. 

Alihudumu katika nafasi mbalimbali za serikali, akiwemo Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (masuala ya sera, bunge, ajira, vijana na walemavu), na baadaye Waziri wa Afya. 

Jenister alikuwa Kada wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama tawala nchini Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

DKT. KIJAZI KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO JIMBO LA KOROGWE MJINI.