Article 19 kushirikiana na JOWUTA kusaidia wanahabari nchini

Mwandishi wetu DmNewsOnline Nairobi SHIRIKA la kimataifa la Article 19, Afrika ya Mashariki, limeahidi kushirikiana na chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania(JOWUTA) kusaidia kuwajengea uwezo wanahabari katika masuala ya utetezi wa sheria za habari, haki za wanahabari na ukatili kwa wanahabari wanawake. Makubaliano ya ushirikiano huo, yamefanyika jijini Nairobi, baina ya JOWUTA na Article 19, mara baada ya mkutano wa taasisi za vyombo vya habari katika nchi za Afrika ya Mashariki,kujadili masuala ya uhuru wa vyombo vya habari, ushirikiano na utetezi wa wanahabari. Naibu Mkurugenzi wa Article 19, Patrick Mutahi akizungumza na Mwenyekiti wa JOWUTA, Mussa Juma alisema taasisi hiyo inatambua changamato za sekta ya habari katika nchi za Afrika ya Mashariki ikiwepo Tanzania na itafanyakazi na JOWUTA. Mutahi amesema, kutokana na changamoto hizo, Article 19 kwa kushirikiana na wahisani wake kadhaa ...