OFISI MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUFANYA MREJESHO WA GHARAMA ZA UCHAGUZI .
Timothy Marko DmNewsOnline
DAR ES SALAAM.
OFISI ya msajili wa vyama vya Siasa Nchini imevitaka Vyama vya Siasa Vilivyo Shiriki Uchaguzi Mkuu October 29,2025 kufanya Mrejesho wa taarifa za Gharama za Uchaguzi.
Akizungumza Leo Machi 10,2026 Naibu Msajili wa vyama vya Siasa Nchini Mohamed Ahmed amesema lengo la kuwakutanisha vyama hivyo nikuweza kutoa Elimu juu ya sheria za Gharama za Uchaguzi .
"Tuliwapa vyama vya Siasa siku 112 kuweza kurejesha fomu za Gharama za Uchaguzi"Amesema Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa
Ahmed Mohamed.
Naye,Katibu Mkuu wa Chama Cha NLD Doyo Hassan Doyo amesema kuwa Warsha hiyo itawasaidia vyama vya Siasa kujua Sheria za Gharama za Uchaguzi.
Aidha,Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Umma Bara Simbo Benson amesema Sheria hiyo itawezesha kufahamu mstakabali wa wagombea hao katika uchaguzi Ujao 2030.
Naye Katibu Mkuu wa Chama Cha ACT Wazalendo Ester Thomas amesema lengo la warsha hiyo ni kutoa Elimu kwa Wagombea juu ya Gharama za Uchaguzi na mchakato mzima wa upatikanaji wa fedha hizo wamezipata wapi Chama kisichotekeleza hayo kitaweza kupata adhabu kwa mujibu wa sheria.
Pia amesema lengo ni kujua fedha hizo umezipata wapi zinatoka wapi na taasisi ipi kwasababu kumekuwa na taasisi za kutoka nje zenye nia ovu. 



Comments
Post a Comment