MAHAFALI YA COHORT YA 11 YA MWANAMKE KIONGOZI, 158 WAHITIMU
Na mwandishi wetu, DmNewsTz
Spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa tanzania mussa azzan zungu amesema bunge litaendelea kufanya maboresho mbalimbali ya sheria zinazolinda haki na ustawi wa wanawake nchini hali itakayosaidia tanzania kuwa na viongozi wengi zaidi wanawake hususani katika ngazi za juu za uongozi
Zungu ameyasema hayo jijini dar es salaam wakati wa hafla ya mahafali ya 11 ya programu ya mwanamke kiuongozi yaliyoandaliwa na taasisi ya waajiri nchini ate yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kiuongozi wanawake ambao ni watumishi kutoka taasisi mbalimbali
Kwa upande wake naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi, ajira na mahusiano rahma kisuo amewataka wahitimu hao kutokuwa vikwazo vya kuwawezesha wanawake wengine katika maeneo yao na badala yake wakawe daraja kwa wengine ili kukuza ushiriki wa wanawake katika maendeleo
Naye Mtendaji Mkuu wa Chama Cha waajili Tanzania (ATE ) Adv. Suzanne Ndomba-Doran amewasihi wahitimu wa Cohort ya 11 kuendelea kushikana mikono na kuwainua wanawake wengine, ili kwa pamoja waweze kufungua fursa zaidi na kufanikisha ndoto za wanawake na wasichana wengi zaidi.
Mwaka huu, Female Future Program imetoa idadi kubwa zaidi ya wahitimu kuliko miaka yote iliyopita (Wahitimu 158). Ikiwa ni ishara ya wazi kuwa programu hiyo inaendelea kukua, kuimarika na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.






Comments
Post a Comment