KASSIM MAJALIWA AFUTURISHA OFISI YA WAZIRI MKUU, AWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA UMOJA NA AMANI.
Timothy Marko DmNews Online
DAR ES SALAAM
WAZIRI MKUU Mstaafu Kassim Majaliwa Majaliwa Amewataka Wananchi kuendeleza misingi ya Amani na utulivu.aliyoasisiwa na watangulizi wetu.
Akizungumza Katika Hafla ya Futari hapo jijini Dar es Salaam Kassim Majaliwa Amewataka Viongozi wa Dini Nchini kudumisha Amani na Umoja na kuwataka kutogawanyika kwa Misingi ya Dini.
"Leo katika Futari hii nimebahatikakuwaona Viongozi wa Madhehebu mbalimmbali wa kisilamu na Wasio Waisilamu hii inamanisha sisi ni Wamoja tusigawanyike katika Misingi ya Dini tuendele kuwa wa moja.
Kwa upande wake Shelkh Mkuu Alhaj Mussa Salum amewataka Wasilamu na wasio waisalamu kuendelea kudumisha Amani iliyopo Nchini nakuwataka Watanzania kutogawanyika katika Misingi ya Dini.


Comments
Post a Comment