DIWANI MASANINGA MKURANGA AFUTURISHA YATIMA , WAZEE NA VIONGOZI MBALIMBALI ,WASEMA NI WATOFAUTI.

  Na Mwandishi wetu,DmNewsonline 

              MKURANGA 

DIWANI wa kata ya kiparang'anda wilayani mkuranga mkoa wa Pwani  Mariam Masaninga amekutana na wenyeviti wa vitongoji na wenyeviti wa vijiji kwa lengo la kuwaeleza kwamba wawe tayari kwa ajili ya kuwatumikia wananchi kwa ajili ya Maendeleo ya kata.

Masaninga amewaeleza viongozi hao kuwa uchaguzi ulishamalizika na kazi iliyoko mbele yao  ni kwenda kwa kuwatumikia wananchi kwa maana ya kutatua kero zao na kuwaletea Maendeleo .

Masaninga ameyasema hayo mapema wiki hii  wakati alipokutana na viongozi hao katika ofisi ya mtendaji kata ya kiparang'anda wilayani mkuranga .

"Nimekuja leo kuwaomba na kuwaeleza kwamba naomba ushirikiano wenu mkubwa na kwamba sasa tunakwenda kufanya kazi kwa ajili ya Maendeleo ya wananchi wetu ndani ya kata ya kiparang'anda na wilaya yetu kwa ujumla ."amesema  

Diwani Masaninga ameewaeleza kuwa endapo watashirikiana kwa pamoja wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Ulega hakuna shaka wilaya hiyo itaendelea kushika Kasi kimaendeleo .

 Katika kikao hicho pia viongozi hao wa vitongoji walimwagiza diwani huyo kumpelekea ujumbe wa kumkumbusha Mbunge wao kwamba yapo mambo alihaidi hivyo wanasubiri.

Akijibu hoja hiyo diwani Masaninga amewaeleza kuwa Mbunge huyo kutokana na mambo kuwa mengi bado hajaaza kwenda kuwatembelea wananchi wake lakini ratiba hiyo Ipo na yupo njiani kuaza ziara hizo za kuwashukuru wananchi baada ya kuchaguliwa tena kuwa Mbunge wa Jimbo la mkuranga .

Wakati huohuo Diwani Masaninga ameweza kufuturisha watoto yatima na viongozi mbalimbali wa kata hiyo  katika kituo Cha kulelea yatima  hao kilichopo ndani ya kata hiyo ya kiparang'anda .

Akizungumza mbele ya watoto hao yatima, na viongozi waandamizi wa kata hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Bakwata wilaya hiyo Sheikh Ismail kirwanda ,Masaninga amewashukuru kwa Mungu kwa kutimiza azma yake hiyo .

Amesema kuwa amefanya jambo ambalo alilikusudia kufanya ukizingatia huu ni mwezi wa haki ambapo wao kama waislam wanahimizwa kukumbuka wajane ,yatima na makundi mbalimbali yenye uhitaji hivyo amejisikia furaha kufikia hatua .

Naye mwenyekiti huyo wa Bakwata wilaya ya mkuranga sheikh Ismail kirwanda amemshukuru na kumpongeza kwa hatua hiyo na kwamba amekuwa mfano wa kuigwa kwa wengine huku akikumbusha viongozi wengine kufanya kile ambacho amelifanya Diwani Masaninga .

 "Tunakupongeza sana kwa hiki ambacho umekifanya na haya ndio maelekezo ya Mola wetu kwamba katika kidogo ambacho unakipata unajaribu kuwakumbuka na wengine na ukifanya hivi unapata thawabu kwa Mungu wetu."amesema sheikh kirwanda.

Viongozi wengine ambao walipata fursa hiyo nao walisema diwani hiyo amepanda mbegu bora na matunda yake atayapata siku ya mwishoni huku wakimtakia Kila la heri katika kazi zake za kuwatumikia wananchi wa kata ya kiparang'anda na wilaya ya mkuranga kwa ujumla.   



Comments

Popular posts from this blog

UONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA WADAIWA SI HALALI NA UMEKOSA DIRA YA KUENDESHA VYAMA VYA WAGANGA WA TIBA ASILI

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.