VIONGOZI WA NCHI MBALIMBALI WAKUTANA KUJADILI MASUALA YA UHARAMIA WA MAJINI
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Uchukuzi Prof.Makame Mbawara amekutana na viongozi kutoka nchi mbalimbali
kujadili changamoto za uharamia wa majini unaofanyika kwenye Bahari ya Hindi.
Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 28,2024 Jijini Dar es salaam Waziri wa Uchukuzi Prof. Mbarawa amesema kuwa mwaka 2007 walikutana na wadau hao ili kujadili uharamia unaofanyika na kuweka mpango mkakati na kanuni zinazohusu usafiri wa majini .
"Mwaka 2018 tulitayarisha mipango na kanuni maalumu za kulinda sekta za usafiri majini ambazo zilitengeneza uangalizi wa kupambana na uharamia kwenye bahari.
Ameongeza kuwa kipindi cha nyuma tulikuwa na waharamia wa kupanda kwenye meli hivyo kwa sasa tunaangalia uharamia wa vitu mbalimbali vikiwemo uharamia wa madawa na uvuvi haramu.
"Mwaka 2023 kulikuwa na watu ambao wanaingia kwenye meli na kufanya Mauaji hivyo hupekelea meli kuzunguka mbali na kusababisha ongezeko la mafuta mengi" amesema Waziri Prof.Mbawara
Waziri wa Uchukuzi PRof.Mbawara ameeleza kwamba maeneo mbalimbali tumeweka mkakati wa kupambana na maharamia hao ili bahari zetu ziwe salama kwani zikiwa salama biashara zinakuwa nzuri na wananchi wanapata bidhaa kwa bei nafuu na kwa urahisi.
"Uharamia ukikithiri kwa wingi meli haziwezi kuingia nchini kwa wakati hivyo na kuleta usumbufu kwa watumiaji na hatimaye bidhaa kuwa juu na adimu",amesema Prof.Mbawara.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa IMO ,Arsenio Dominguez ameongeza kuwa tunaongeza ulinzi na usalama kwenye meli zote baharini ili kuimarisha shughuli zote zinazofanyika baharini ,hata hivyo tunashukuru kwa kuweza kushiriki mkutano wa Saba wa Juuu wa Utekelezaji wa kujadili na kutatua changamoto zinazojitokeza kwenye vyombo vya majini.
Comments
Post a Comment