CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA VITONGOJI
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
Chama cha Mapinduzi CCM kimeshinda nafasi 12,150 (99.01%) kwenye nafasi ya Wenyeviti wa Vijiji katika Vijiji vyote 12271 vilivyofanya Uchaguzi huku CHADEMA ikishinda nafasi 97 (0.79%).
Akitangaza matokeo ya jumla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usiku huu, Waziri wa TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa amesema ACT Wazalendo imeshinda nafasi 11 (0.09%) , CUF imeshinda nafasi 10, NCCR , UMD na ADC wameshinda nafasi moja kila Chama.
“Vijiji tisa havijafanya Uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo vya Wagombea baada ya uteuzi” — Mchengerwa.
Chama cha Mapinduzi 'CCM' Pia kimeshinda nafasi 62728 sawa na asilimia 98.26 kwenye nafasi ya Wenyeviti wa Vitongoji Nchini ikifuatiwa na CHADEMA ambayo imeshinda nafasi 853 (1.34%) katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana.
ACT Wazalendo imeshinda nafasi 150 (0.23%) , CUF imeshinda nafasi 78, NCCR nafasi 10, UDP nafasi 6, UMD nafasi mbili na ADC wameshinda nafasi moja.
Comments
Post a Comment