CCM YAAHIDI KUWATUMIKIA WANANCHI PASIPO KUCHOKA
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
KATIBU wa NEC Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makala amesema kutokana na ushindi tutaenda kuwatumikia wananchi pasipo kuchoka kwani ushindi wa Chama unatokana na kuaminiwa na wananchi.
Akizungumza na wanahabari Novemba 29,20240 katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba Jijini Dar es Salaam, CPA. Makalla amesema, ushindi wa vyama vyote unatokana na wingi wa kura za wananchi.
Aidha amesema uhalali wa ushindi wao umetokana na wananchi kwa kazi nzuri ambayo chama hicho imekuwa ikifanya hususani katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na utatuzi wa kero kwa wananchi wake.
" CCM inatambua kuwepo kwa changamoto katika uchaguzi huu uliopota wa Serikali za Mitaa, hivyo amewasisitiza viongozi wa vyama vyote vya siasa kushirikiana ili waweze kutatua changamoto hizi zisijirudie katika chaguzi zijazo",amesema CPA Makala.
CPA Makala amesema kwamba tunatambua kwamba zipo changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika uchaguzi huu lakini tushirikiane vyama vya siasa ambao ni wadau
kuhakikisha na sisi tunakuwa sehemu ya kutatua changamoto hizo hususani katika wakati wa uteuzi wa wagombea.
Alieleza kuwa tujitahidi kutoa elimu kwa wagombea wetu hususani katika ujazaji wa fomu kila mmoja kujaza fomu kwa umakini na usahihi na kufanya hivyo kutaondoa sintofahamu kwa wahusika
Comments
Post a Comment