Posts

Showing posts from November, 2024

EMIRATES LAUNCHES CURATED CONTENT COLLABORATION WITH SPOTIFY

Image
DmNewsOnline Emirates has launched a new collaboration with spotify the world’s most popular audio-streaming subscription service. Offering customers a wide array of podcasts and playlists in the sky, Spotify can be enjoyed by all customers on their personal inflight entertainment seatback system, ice. Catering to Emirates’ global customer base, the curated content from Spotify will include a range of popular music playlists, as well as top podcasts in English, Portuguese, Tagalog and German, with more languages including Spanish and Hindi to be added in 2025. New podcasts and music will be added regularly to complement Emirates’ existing library of more than 3500 hours of global music and thought-provoking conversations. Emirates’ customers can now explore Spotify’s diverse podcast library with over 140 episodes of business, sports, entertainment and true crime, featuring voices of renowned personalities such as  What Now? with Trevor Noah  – as the comedian has c...

CHEERS AS BREWERS SHINE AT EYA 2024

Image
                         DmNewsOnline Yesterday evening Friday November 29 Tanzania Breweries Plc emerged the Overall winner for EYA 2024.  Runners Up were Barrick North Mara Gold Mine Limited and Tanzania Ports Authority respectively.  The evening was filled with mixed feelings as the winners of the Employer of the Year Award(EYA) 2024 walked away with trophies reflecting their outstanding Human Resources management practices. Organised by the Association of Tanzania Employers (ATE), this year the annual Award was made more exciting with the addition of two criteria namely, Occupational Health and Safety plus HIV& AIDS Response. He award giving ceremony was graced by the Deputy Prime Minister and Minister for Energy Hon. Dr. Doto Mashaka Biteko MP who said he was happy  to congregate at EYA  for the first time and conveyed greetings from the Vice President Hon. Dr . Philip Isdor Mpango He tha...

Rais Samia Suluhu Hassan: Aiongoza Tanzania Kuongoza Katika Biashara Afrika mashariki.

Image
Na Mwandishi wetu, DmNewsOnline Uongozi wa kimaono wa Rais Samia Suluhu Hassan umeendelea kuipa Tanzania mafanikio makubwa katika biashara za kikanda, na kuthibitisha nafasi ya nchi kama kiongozi wa Afrika Mashariki. Hili lilidhihirishwa hivi karibuni wakati Rais wa Kenya, William Ruto, alipokiri waziwazi katika maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwamba Kenya imesalia nyuma kibiashara huku Tanzania ikipiga hatua kubwa chini ya uongozi wa Rais Samia.   Matokeo ya uongozi huu yameonekana wazi zaidi Novemba 2024, Tanzania ilipoipita Kenya na kuwa chanzo kikuu cha uagizaji wa bidhaa za Uganda kutoka Afrika. Benki ya Uganda iliripoti kuwa katika mwaka wa fedha ulioishia Juni 2024, Uganda iliagiza bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 4.17 (KSh bilioni 540) kutoka Afrika, ambapo Tanzania ilichangia asilimia 42.56 ya jumla hiyo. Kwa kulinganisha, Kenya ilichangia asilimia 19.55 tu, huku Afrika Kusini ikiwa na asilimia 6.43.   Mafanikio haya yanaonye...

KIKAO CHA DHARURA CHAOTA MBAWA.

Image
Na Mwandishi wetu,NewsOnline Kukosa kufanya mkutano wa dharura ulioandaliwa kwa tarehe 29 Novemba, 2024, na CHADEMA, chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, kimeibua uvumi wa mgawanyiko mkubwa ndani yake. Kukosa kufanyika kwa mkutano huu, ambao umefichwa katika siri, kinaonyesha kuna matatizo yasiyo ya hadharani kati ya viongozi wake wakuu, hasa kati ya kambi ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na ile ya Naibu Mwenyekiti Tundu Lissu. Mizozo ya Ndani: 1. Uongozi Mdogo Mdogo: Chanzo karibu na chama kinasema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya makambi haya, kila moja ikiwa na maono tofauti kuhusu mustakbali wa chama. Hii inaaminika kuwa imesababisha kutatuzi la maamuzi, hivyo kufanya mkutano huu usifanyike. 2. Ukosefu wa Sera Mpya: Kwa kutokuwa na sera au mikakati mipya ya kujadili, ajenda ya mkutano inasemekana ilikuwa nyembamba, inaonyesha jitihada za chama kujiremba baada ya kushindwa tena katika mzunguko wa uchaguzi. Huenda hii ndiyo sababu mkutano ulipostiwa au uliwekwa kando hadi hakuna muda ...

CCM YAAHIDI KUWATUMIKIA WANANCHI PASIPO KUCHOKA

Image
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline DAR ES SALAAM  KATIBU wa NEC Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Taifa CPA Amos Makala amesema kutokana na ushindi tutaenda kuwatumikia wananchi pasipo kuchoka kwani ushindi wa Chama unatokana na kuaminiwa na wananchi. Akizungumza na wanahabari Novemba 29,20240 katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba  Jijini Dar es Salaam, CPA. Makalla amesema, ushindi wa vyama vyote unatokana na wingi wa kura za wananchi. Aidha amesema uhalali wa ushindi wao  umetokana na wananchi kwa kazi nzuri ambayo chama hicho imekuwa ikifanya hususani katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na utatuzi wa kero kwa wananchi wake. " CCM inatambua kuwepo kwa changamoto katika uchaguzi huu uliopota wa Serikali za Mitaa, hivyo amewasisitiza viongozi wa vyama vyote vya siasa kushirikiana ili waweze kutatua changamoto hizi zisijirudie katika chaguzi zijazo",amesema CPA Makala. CPA Makala amesema kwamba tunatambua kwamba zipo changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika uchaguzi huu lakini...

MAMLAKA USAFIRISHAJI MAJINI BARANI AFRIKA ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUBORESHA HUDUMA

Image
Na mwandishi wetu,DmNewsOnline DAR ES SALAAM    JUMUIYA  ya Mamlaka za Usimamizi wa Usafiri majini Barani Afrika zimetakiwa kushirikiana na kuungana ili kuimarisha usalama wa sekta ya usafirishaji majini na hivyo kuchochea maendeleo ya Uchumi katika nchi husika. Wito huo umetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (Novemba 29, 2024) wakati akifungua Kongamano na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Jukumuiya ya Mamlaka za Usimamizi na Usafirishaji Majini Barani Afrika unaofanyika kwa siku tatu, Jijini Dar es Salaam. Dkt. Biteko amewashauri washiriki kutumia mkutano huo kama fursa ya kubuni na kupanga mikakati mipya ya kuelekea katika mafanikio kupitia sekta hiyo ambapo amesisitiza kuwa ushirikiano miongoni mwa washiriki na kujadiliano juu ya kuwezesha masuala mbalimbali na sekta ya usafirishaji litakuwa suluhisho la changamoto mbalimbali zilizopo. “Kila mmoja wetu atumie fursa ya mkutano huu kujiwekea malengo yatakayo tuwezesha kufikia azima ya kuboresh...

CCM YASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA VITONGOJI

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline Chama cha Mapinduzi CCM kimeshinda nafasi 12,150 (99.01%) kwenye nafasi ya Wenyeviti wa Vijiji katika Vijiji vyote 12271 vilivyofanya Uchaguzi huku CHADEMA ikishinda nafasi 97 (0.79%). Akitangaza matokeo ya jumla ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usiku huu, Waziri wa TAMISEMI, Mohammed Mchengerwa amesema ACT Wazalendo imeshinda nafasi 11 (0.09%) , CUF imeshinda nafasi 10, NCCR , UMD na ADC wameshinda nafasi moja kila Chama. “Vijiji tisa havijafanya Uchaguzi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo vifo vya Wagombea baada ya uteuzi” — Mchengerwa. Chama cha Mapinduzi 'CCM' Pia kimeshinda nafasi 62728 sawa na asilimia 98.26 kwenye nafasi ya Wenyeviti wa Vitongoji Nchini ikifuatiwa na CHADEMA ambayo imeshinda nafasi 853 (1.34%) katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika jana. ACT Wazalendo imeshinda nafasi 150 (0.23%) , CUF imeshinda nafasi 78, NCCR nafasi 10, UDP nafasi 6, UMD nafasi mbili na ADC wameshinda nafasi moja.

VIONGOZI WA NCHI MBALIMBALI WAKUTANA KUJADILI MASUALA YA UHARAMIA WA MAJINI

Image
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline DAR ES SALAAM  WAZIRI wa Uchukuzi Prof.Makame Mbawara amekutana na viongozi kutoka nchi mbalimbali  kujadili changamoto za  uharamia wa majini  unaofanyika kwenye Bahari ya Hindi. Akizungumza  na waandishi wa habari Novemba 28,2024 Jijini Dar es salaam  Waziri wa Uchukuzi Prof.  Mbarawa amesema kuwa mwaka 2007 walikutana na wadau hao ili kujadili uharamia unaofanyika na kuweka mpango mkakati na  kanuni zinazohusu usafiri wa majini . "Mwaka 2018 tulitayarisha mipango na kanuni maalumu za kulinda sekta za usafiri majini ambazo zilitengeneza uangalizi  wa kupambana na uharamia kwenye bahari.  Ameongeza  kuwa kipindi cha nyuma tulikuwa na waharamia wa kupanda kwenye meli hivyo kwa sasa tunaangalia uharamia wa vitu mbalimbali vikiwemo uharamia wa madawa na uvuvi haramu. "Mwaka 2023  kulikuwa na watu ambao wanaingia kwenye meli na kufanya Mauaji hivyo hupekelea meli kuzunguka mbali na kusababisha ongez...

LISSU AVUJISHA SIRI, ANGUKO LA CHADEMA

Image
Na Mwandishi wetu, DmNewsOnline DAR-Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, Tundu Lissu ameibuka na kile ambacho ni kiashiria cha anguko la chama hicho. Lissu ambaye siku za karibuni amekuwa akiibua mambo mazito ndani ya CHADEMA ikiwemo tuhuma za rushwa kwa sasa inaonekana amekata tamaa na mwelekeo wa chama hicho kwa sasa. huu ni ujumbe wake katika kundi sogozi la WhatsApp chadema Kaskazini.  "Hii hoja haina mashiko yoyote kwenye logic na kiuhalisia. Vyama vya siasa hushiriki uchaguzi kwa kutegemea mazingira ya kisiasa ya nchi husika na malengo ya chama chenyewe. "Chama cha siasa chenye malengo ya kushika dola ili kufanya mabadiliko ya msingi katika siasa, uchumi na jamii lazima kipiganie kwanza mabadiliko ya msingi ya mfumo wa uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki. "Kisipofanya hivyo, badala yake kikaamua kushiriki kila aina ya uchaguzi, basi hakitakuwa na future yoyote. Kitakufa a natural death. Mifano ni mingi katika ...

MWANACHAMA CHADEMA AWABABUA LISSU,MBOWE., ATAKA WAKIACHE CHAMA

Image
Na Mwandishi wetu, DmNewsOnline SINGIDA Mpasuko ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umeendelea kutamalaki huku chanzo kikuu kikitajwa kuwa ni viongozi wakuu wa chama hicho kuyapa kisogo majukumu na vipaumbele vya chama huku wakiangalia fursa za kushibisha matumbo yao. Hali hiyo, inatajwa na baadhi ya wanachama wa chama hicho kuwa chanzo kikuu cha wao kukosa mwelekeo na kupoteza matumaini kuanzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa hadi Uchaguzi Mkuu ujao. Miongoni mwa viongozi ambao wanatajwa kutotabirika ni Makamu Mwenyekiti wa chama Bara, Tundu Lissu ambaye imedaiwa ni hodari wa kulalamika, lakini uwezo wa kutenda ni sufuri. "Wakati Taifa linajiandikisha kupiga kura kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, Tundu Lissu alikuwa Ulaya. "Wakati wa kampeni, alikuwa bize kutuambia ukweli kwamba chama chake hakikujipanga. "Leo, siku ya uchaguzi, hayupo.Hodari wa kulalamika, lakini bingwa wa kutotenda. Huu ndio udhaifu wa uongozi wa CHADEMA. "Wameshindwa kutekelez...

MBUNGE JIMBO LA MBOGWE APIGA KURA ,KUCHAGUA VIONGOZI ,SERIKALI ZA VIIJIJI NA VITONGOJI.

Image
     Na  Mwandishi Wetu,DmNewsOnline  MBOGWE _GEITA MBUNGE wa Jimbo la Mbogwe mkoani Geita Nicodemas Maganga leo ameungana na wananchi wa jimbo hilo  kushiriki zoezi la kupiga kura kwa lengo la kuchagua viongozi wanaofaa kuongoza kwenye ngazi za serikali ya kijiji na vitongoji . Maganga amepiga kura hiyo katika kituo kilichopo shule ya sekondari Masumbwe huku akipongeza kwa namna zoezi hilo linavyokwenda na wananchi wanavyojitokeza na kudumisha amani na utulivu. Mbunge Maganga ameyasema hayo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura.ambapo amesisitiza wananchi kuendelea kujitokeza kwenye vituo mbalimbali ili kutimiza haki yao ya msingi ya  kidemokrasia ya kuchagua viongozi watakao wafaa . "Nikweli ndugu zangu waandishi kama mnavyojua leo ni siku ya mapumziko  kwa nchi nzima, kwa lengo la kupiga kura ili wananchi waweze kupata viongozi watakao watumikia na kuwaletea maendeleo katika maeneo yao.hivyo mimi kama mbunge nam...