RAIS DKT .SAMIA ANATARAJIA KUONGOZA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI BEIJING CHINA.



Na  Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuongoza  mkutano wa Kilele wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika kuanzia Septemba 4 hadi  2024 Jijini Beijing, China.

Hayo  yamesemwa  Leo Agosti 31,2024 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo (MB)  amesema kuwa Dkt Samia atashiriki mkutano huo kufuatia mwaliko wa  Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Xi Jinping.

" Ushiriki wa Rais Dkt.  Samia kwenye mkutano wa kilele wa FOCAC unalenga kuendeleza  kudumisha ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na China ambao mwaka huu umetimiza miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili",amesema

 Aidha kutokana na  makubaliano ya Serikali ya China namna ya kuendelea kuongeza ushirikiano katika maeneo ya kipaumbele kwa maendeleo ya pande ya Taifa ikiwemo katika sekta ya miundombinu, mifumo ya chakula, biashara na uwekezaji, kubadilishana ujuzi, upatikanaji wa nishati safi na salama na kusaidia ujenzi wa uchumi wa kidijitali. 

Aidha Waziri Kombo ameongeza kuwa ziara hiyo inaenda  kuibua fursa mpya za ushirikiano kwa manufaa ya pande zote mbili pamoja na kutangaza maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya Sita ya sera na sheria katika sekta ya biashara na uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi kutoka nchini humo.

Vilevile  Serikali ya China imemteua Rais Dkt. Samia kuhutubia kwenye hafla ya ufunguzi wa mkutano huo wa Kilele wa wakuu wa Nchi na Serikali wa FOCAC itakayofanyika  Septemba 4 hadi 6, 2024, akiiwakilisha Kanda ya Afrika Mashariki, huku kauli mbiu ikiwa “Kushirikiana ili Kuendeleza Usasa na Kujenga Jamii Bora ya China na Afrika kwa Mustakabali wa Pamoja"

Pamoja na hayo pia amesema kuwa, ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo utaongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ataungana na wakuu wa Nchi na Serikali ,wenzake kutoka Nchi zaidi ya 40 kati ya 54 za Bara la Afrika kushiriki Mkutano huo.

Hata hivyo ameongeza kuwa jukwaa la FOCAC lilianzishwa mwaka 2000 na Jamhuri ya watu wa China kwa lengo la kukuza ushirikiano na maendeleo ya pamoja kati ya China na Afrika,  ambapo tangu kuanzishwa kwake jumla ya mikutano  nane ya Kilele  ya Wakuu wa Nchi na Serikali  imefanyika.

"Mikutano hiyo hufanyika kila baada ya miaka mitatu kwa kubalishana kati ya China na nchi moja ya Afrika, mkutano huu wa 9 wa FOCAC utafungulia na Xi Jinping, Rais wa Jamhuri ya Watu wa China ambapo, hotuba yake ya ufunguzi itatoa uelekeo wa China katika uhusiano wake na nchi za Afrika, 

Aliendelea kwa kusema kwamba viongozi mbalimbali watashiriki katika mkutano huo ikiwa ni pamoja na Antonia Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Moussa Faki, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika watashiriki Mkutano huo.

" Mada ambazo zinaenda kujadiliwa ni pamoja na Utawala wa Nchi, Mpango wa Miundombinu na Uwekezaji, Maendeleo ya Viwanda na Kilimo cha Kisasa na Amani na Usalama, kwa upande wa Tanzania utajikita kwenye mada ya Maendeleo ya Viwanda na Kilimo cha Kisasa mada hiyo imezingatia Mpango wa Maendeleo wa Tatu wa Miaka Mitano, ambao ndiyo mpango wa mwisho wa utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya 2025.

Pia Tanzania inatarajia kuwasilisha miradi mbalimbali ikiwemo mipya na ile ambayo haikuweza kutekelezwa kwenye mpango uliopita wa FOCAC kwa sababu mbalimbali, ili iweze kutekelezwa chini ya mpango kazi wa FOCAC kwa kipindi cha 2025-2027 kwa kupatiwa fedha za mkopo nafuu na msaada.

 Miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi wa Mtandao wa Mawasiliano Vijijini wa awamu ya Pili, ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme wa Kv 400 wa awamu ya Pili na Tatu , Ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) wa awamu ya Pili na Ujenzi wa Barabara za Zanzibar Zenye Urefu wa Kilomita 277.7

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025