WAZIRI MAVUNDE ATEMBELEA MRADI WA LINDI JUMBO


 Na Mwandishi Wetu, DmNewsOnline 
LINDI

WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Desemba 28, 2023 ametembelea mradi wa Lindi Jumbo Limited uliopo Wilaya ya Ruangwa Mkoa wa Lindi kwa lengo la kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa mgodi wa madini ya kinywe (graphite)

Awali akielezea maendeleo ya ujenzi wa mgodi huo, Meneja wa Mradi, Chediel Mshana ameeleza kuwa mradi huo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mtambo wa uchenjuaji umefikia zaidi ya asilimia 90 ambapo uzalishaji wa   madini ya kinywe unatarajia kuanza mapema Machi, 2024.

Ziara hii ni sehemu ya ziara za Waziri Mavunde zenye lengo la kukagua shughuli za uchimbaji wa madini nchini sambamba na kutatua changamoto mbalimbali.

Katika ziara yake ameambatana na Mkurugenzi wa Ukaguzi wa Migodi na Mazingira, Mhandisi Henry Mditi kutoka Tume ya Madini na Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Lindi, Dickson Joram



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025