VINGOZI WA DINI WATAKA TIP ISAMBAZE ELIMU DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA VIJIJINI
Na Paul Kayanda,DmNewsOnline
KAHAMA
VIONGOZI wa madhehebu ya Dini Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga,wamebainisha changamoto mbalimbali zinazokwamisha juhudi za kusambaza Elimu dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia vijijini ikiwemo shida ya usafiri ili kuwafikia walengwa hao.
Viongozi hao wamesema kuwa,mara nyingi vitendo vya ukatili wa kijinsia hufanyika katika maeneo ya vijijini ambako hakuna msaada wowote tofauti na maeneo ya mijini ambako ambako pia matukio hayo yameshamiri hivyo viongozi wametumia fursa hiyo kuliomba Shirika la TIP pamoja na Serikali kuhakikisha kuwa wanasambaza Elimu katika maeneo ya Vijijini.
Ally Athumani Ally pamoja na viongozi wengine wamesema hayo Leo Disemba 28,2023 kwenye kikao cha uwasilishaji wa taarifa za kupinga na kuzuia ukatili wa kijinsia kilichojumuisha viongozi wa madhehebu mbalimbali katika makundi ya viongozi wa dini Kwa maana Taassisi za TEC, CPCT, BAKWATA pamoja na CCT kilichofanyika katika Manispaa hiyo.
Aidha Viongozi wa Madhehebu ya Dini wamesema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa vyombo vya usafiri ili kuwafikia walengwa pamoja na mambo mengine nivyo wametumia nafasi hiyo kuwasilisha kwa Shirika hilo na kuiomba Serikali kuangalia namna ya kuweza ili kufanikisha usambazaji wa Elimu hiyo hali ambayo itasaidia kutokomeza vitendo vya Ukatiri wa Kijinsia.
Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Kahama Swahiba Chem Chem akizungumza kwa niaba ya Serikali amewapongeza na kulishukuru Shirika la TIP kwa kuwahusisha viongozi wa Madhehebu ya Dini ili kuhakikisha Elimu dhidi ya vitendo vya ukatili wa Kijinsia inasamba kwa kasi katika maeneo mbalimbali nchini.
Aidha Ofisa Ustawi wa Jamii ameliomba Shirika hilo lisiishie katika makundi hayo pekee bali lihusishe na makundi mengine muhimu yenye nguvu na ushawishi kwa Jamii
Comments
Post a Comment