MBUNGE WA USHETU DKT. CHEREHANI AHADI KUEZEKA NYUMBA YA PADRE .KIGANGO CHA KISUKE.


Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline 

MBUNGE  wa jimbo la Ushetu mkoani shinyanga  Emmanuel Cherehani ameahidi kutoa mbao 300 zenye thamani ya shilingi 1,350,000 kwaajili ya kuezeka nyumba ya mapadre katika kanisa la mtakatifu Karolilwanga kigango cha Kisuke parokia ya Nyamilangano.

Ahadi hiyo ametoa Leo Disemba 25 ,2023 katika Ibaada ya sikukuu ya Krismas ambapo  Cherehani amesema, katika kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo ni vyema pia waumini kuzaliwa upya katika Imani kwa kusali na kujenga kanisa  kwani uwepo wa nyumba ya mapadre utarahisisha utoaji wa huduma za kiroho.


Pia  Cherehani amewataka wananchi wa Ushetu kudumisha amani na upendo kwani kusherehekea Krismas ni kukumbuka kuwa tunae Kristo anaetaka tusali na tusitende dhambi hivyo amewasihi kusherehekea sikukuu kwa utulivu na amani.

Akizungumza kwa niaba ya waumini  Mwenyekiti wa kigango hicho Grace Kiondo amemshukuru mbunge wa jimbo la Ushetu kwa moyo wa kujitolea, ambapo ameahidi kuwa Wataendelea kumpa  ushirikiano katika kutimiza majukumu yake ya maendeleo kwa Wananchi wa jimbo hilo.

Kigango cha Kisuke kipo katika Parokia ya mtakatifu Petro na Paulo Mitume Nyamilangano, ambapo waumini walijenga jengo la nyumba ya mapadri lakini walishindwa kukamilisha upauaji nyumba hiyo.





Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025