KESI YA PAULINE GEKUL YAFUTWA,BABATI

Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline 

MAHAKAMA ya wilaya ya Babati imeifutilia mbali kesi ya ukatili iliyokuwa inamkabili mbunge wa jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul kuhusu tuhuma za unyanyasaji kwa kijana Hashim Ally.

Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 27, 2023, na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya Babati, Victor Kimario na kusema ameifuta baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.


Kesi hiyo ilifunguliwa kupitia kwa wakili Peter Madeleka chini ya kifungu cha 128(2) na (4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Ambapo kwa upande wake Wakili Madeleka amesema hawajakubaliana na maamuzi hayo na kwamba watakata rufaa.

 Kesi hiyo dhidi ya Mbunge Paulina Gekul ilifunguliwa na wakili huyo kwa kushirikiana na wenzake wakidai alimfanyia kitendo cha ukatili kijana huyo kwa kumuingizia chupa sehemu ya haja kubwa.


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025