CCM MAGOMENI DAR ES SALAAM YAJIPANGA KIMKAKATI KUWATUMIKIA WANANCHI
Na Mwandishi Wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Magomeni Mohamed Mwinyi amesema katika kuendelea kujiweka vizuri kiutendaji na kutatua baadhi ya changamoto za wananchi kimeweza kufanya vikao mbalimbali kuanzia kwa viongozi wa Mabalozi hadi wale wa Matawi lengo likiwa ni kujua uhai wa chama na hasa kinapoelekea mwishoni mwa mwaka.
Hayo yalitanabaishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho wakati akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Jijini Dar es Salaam uku akisema wako vizuri na wamejipanga kwa ajili ya chaguzi zijazo.
Amesema Chama kimekuwa karibu na wananchi wake lakini kubwa zaidi likiwa ni kujua changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na kufanya vikao kwa ajili ya kujua uhai wa chama.
"Lakini pia kujiandaa na chaguzi za Serikali za Mitaa, kuweka mahusiano mazuri kati ya Wananchi na viongozi wao kwani bila kufanya hivyo mnaweza kuambulia matokeo msiyo yatarajia," alisema Mwenyekiti Mwinyi.
Kiongozi huyo alisema kuwa katika kuhakikisha wanawatendea haki wananchi, walifanikiwa kufanya vikao vya Kikatiba vyote na kuvimaliza kikiwemo kile cha Halmashauri Kuu na Kamati za Siasa.
"Lakini sikuishia hapo badala yake nimefanya mikutano yote yaani ya Jumuia zote za Chama na kuzimaliza na pia ziara kwenye Matawi yote matano na kumalizia kwa Mabalozi na baada ya hapa sasa tutaingia kwenye mikutano ya nje" amesema.
Kuhusu changamoto, alisema "awali kulikuwa na malalamiko yakuwa malipo madogo kwa wale waliovunjiwa kwenye mradi huku wengine wakisusa na kusema kuwa malipo madogo badaye tulikutana nao akiwemo Mkuu wa Wilaya pamoja na Diwani wa Kata Noordin Butembo na baada ya hapo Mkuu huyo alilichukua suala hilo.
"Lakini kwa upande wa wale wa mwanzo bado ila napendekeza kuwa viongozi wa juu waangalie uwezekano hata wa kuwalipa kifuta jasho," amesema Mwenyekiti Mohamed.
Hata hivyo alitamba kuwa hawana tatizo la taka kwani wanagari ambao uzoa taka hizo kwa siku sita na kupunzika siku moja, tofauti na yalivyo maeneo mengine.
Comments
Post a Comment