HIFADHI YA TAIFA RUAHA YAWAITA WANANCHI KUSHEREHEKEA MIAKA 60 YA KUAZISHWA KWAKE.

Na Eliasa Ally ,DmNewsOnline IRINGA MKUU wa Hifadhi ya Ruaha Mkoa wa lringa, Godwel Ole Meing’ataki Amewataka Wananchi kwenda kutembelea hifadhi ya Taifa Ruaha kama Moja ya Kuunga mkono sherehe za maadhimisho ya miaka 60 tangu uwepo wa Hifadhi hiyo. Akizungumza na wandshi wa Habari mwishoni mwa wiki katika maandalizi ya kulekea maadhimisho hayo ya mika 60 ya hifadhi hiyo . Amesema kuwa sherehe za maadhimisho hayo zitatanguliwa na shughuli mbali mbali za kijamii pamoja na elimu juu ya umuhimu wa Hifadhi. Ameongeza kuwa Hifadhi imejipanga kuimarisha uhusiano na jamii mbalimbali, ikiwemo watu wenye ulemavu, kwa lengo la kuwapatia fursa ya kutembelea hifadhi hiyo pamoja na kutoa msaada kwa familia zenye mazingira magumu “Nitumie fursa hii kuwakaribisha Watanzania wote, hususani wakazi wa Iringa, katika maadhimisho ya miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo yatafanyika kuanzia octoba 1 hadi 7 2024, amb...