HIFADHI YA TAIFA RUAHA YAWAITA WANANCHI KUSHEREHEKEA MIAKA 60 YA KUAZISHWA KWAKE.
Na Eliasa Ally ,DmNewsOnline
IRINGA
MKUU wa Hifadhi ya Ruaha Mkoa wa lringa, Godwel Ole Meing’ataki Amewataka Wananchi kwenda kutembelea hifadhi ya Taifa Ruaha kama Moja ya Kuunga mkono sherehe za maadhimisho ya miaka 60 tangu uwepo wa Hifadhi hiyo.
Akizungumza na wandshi wa Habari mwishoni mwa wiki katika maandalizi ya kulekea maadhimisho hayo ya mika 60 ya hifadhi hiyo .
Amesema kuwa sherehe za maadhimisho hayo zitatanguliwa na shughuli mbali mbali za kijamii pamoja na elimu juu ya umuhimu wa Hifadhi.
Ameongeza kuwa Hifadhi imejipanga kuimarisha uhusiano na jamii mbalimbali, ikiwemo watu wenye ulemavu, kwa lengo la kuwapatia fursa ya kutembelea hifadhi hiyo pamoja na kutoa msaada kwa familia zenye mazingira magumu
“Nitumie fursa hii kuwakaribisha Watanzania wote, hususani wakazi wa Iringa, katika maadhimisho ya miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambayo yatafanyika kuanzia octoba 1 hadi 7 2024, ambapo ndio itakuwa kilele cha sherehe hizo.
Amesema kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho hayo Waziri wa Mali Asili na utalii Balozi Dkt. pindi Chana ambaye atahitimisha shughuli hiyo kwa kuzindua rasmi utalii wa puto.
Kuwa huduma hii mpya ya utalii wa puto inalenga kuwavutia watalii zaidi katika hifadhi hiyo kwa kuwapa fursa ya kufurahia mandhari ya kuvutia ya Ruaha kutoka angani.
Alisema Katika maadhimisho hayo, Hifadhi ya Ruaha itashirikiana na wadau mbalimbali wa mkoa wa Iringa, wakiwemo viongozi wa kimila na kidini, kwa kufanya ziara maalumu za kutembelea hifadhi hiyo.
Meing’ataki alieleza kuwa ziara maalum kwa Chifu wa kabila la Wahehe na viongozi wake wa kimila, pamoja na viongozi wa dini, zimepangwa ili kuongeza uelewa na ushirikiano katika uhifadhi wa mazingira.
Pia, amesema kutakuwa na kongamano maalum la miaka 60 ambalo litajikita katika kujadili historia ya hifadhi hiyo, mafanikio yaliyopatikana na changamoto zilizopo, sambamba na kutoa mapendekezo ya namna ya kuimarisha uhifadhi.
Hifadhi hiyo pia imeandaa ziara kwa watu wenye ulemavu kutoka mkoa wa Iringa ili wapate fursa ya kutembelea na kujionea vivutio vilivyomo katika hifadhi ya Ruaha.
Comments
Post a Comment