CCM KIBAHA MJI YATOA TAMKO LA KULAANI VITENDO VYA MAUAJI YA BODA NA ALBINO

Na Victor Masangu,DmNewsOnline KIBAHA CHAMA cha mapinduzi Wilaya ya Kibaha mjini (CCM) kimelaani vikali vitendo vya matukio ya mauaji ya madereva wa boda boda yanayoendelea katika maeneo mbali mbali. Akitoa tamko hilo katika kikao cha halmashauri kuu ya chama Mwenyekiti wa (CCM) Mwalimu Mwajuma Nyamka alisema kwamba wameamua kwa pamoja kutoa tamko hilo kutoka na kukithiri kwa matukio hayo. Nyamka amesema kwamba matukio hayo ya unyang'anyi wa kuporwa pikipiki na kufanya mauaji yanafanywa na kikundi cha majambazi. Amefafanua kuwa hivi karibuni kumetokea tukionla Katibu wa CCM tawi la Miswe kata ya Mbawa ambapo ndugu Sitaki Pazi kuporwa pikipiki na kuuwawa. Pia Mwenyekiti Nyamka amesema kwamba chama pia kinalaani vikali mauaji ya kikatili aliyofanyiwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) Asimwe Novat mwenye umri wa miaka miwili na nusu. Katika hatua nyingine chama cha mapinduzi kimetoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa hatua ambazo limeanza kuzichukua na kuwatia mba...