WANANCHI WATAHADHARIWA NA VIVIMBE VINAVYOJITOKEZA KWENYE MWILI.

  Timothy Marko DmNews online 

          DAR ES SALAAM.

WANANCHI wametakiwa  kufanya Uchunguzi wa kiafya Mara kwa Mara Juu ya Kuvimba unaojitokeza kwenye Mili yao, ilikuweza kuondokana na Tatizo la Ugonjwa wa Saratani.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam katika Semina ilioyowakutanisha  Waandishi wa habari na  wahariri wa Vyombo vya Habari Meneja Huduma za Uchunguzi wa Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt.Maguhwa Stephano amesema Takwimu za Taasisi hiyo zilizofanywa 2024 zilionesha kuwa kati ya Wagonjwa 900walihudhuria Taasisi hiyo walibainika kuwa na Ugonjwa wa Saratani huku kati yao 100 walibainika kuwa na Dalili za Ugonjwa huo watano kati yao walikuwa Wanawaume Ambapo Wanaume hao, walibainika kuwa kuwa Saratani ya vivimbe kwenye matiti.

"Tunawahimiza Wananchi kufanya Uchunguzi wa Uvimbe wowote unaojitokeza kwenye mwili  kwani Ni chanzo kikuu cha Saratani"Amesema Meneja Huduma za Uchunguzi wa Saratani Dkt.Maghua  Stephano.
 
Dkt.Maghua Ameongeza kuwa Saratani inatibika kwa Wepesi Endapo itawahiwa  Mapema

Amesisitiza Kuwa Nivyema Wananchi kwakawa natahadhari na Utumiaji wa Vilevi Vikali namatumizi sigara pamoja na shisha kama mtindo wa Maisha kwani ndio kichocheo kikuu cha Saratani.

"Uvimbe unaojitokeza kwenye mwili Ambao unaojitokeza kwenye mwili kwa ghafla , Uvimbe huo hauumi hiyo nidalili za Awali za Ugonjwa wa Saratani " Alisisitiza Dkt.Maguhwa .

Naye Shujaa na Mhanga wa Ugonjwa wa Saratani Batuli Ramadhani amesema Aligundulika kuwa na Ugonjwa wa Saratani ya MatitiMwaka 2004  nakuanza kupata Vivimbe Vidogo kwenye Matiti.

"Nikaenda Hospital ya Taifa ya Muhimbili na kuhamishwa Taasisi ya Saratani Ocean Road kufanyiwa Uchunguzi"Amesema Batuli Ramadhani.

Mhanga  wa Ugonjwa wa Saratani Aliiomba SERIKALI kupunguza Gharama za Matibabu kutokana Hali Upatikanaji wa tiba hiyo ni Ghali.

Amesema Gharama za Uchunguzi wa Mzunguko Moja wa Tiba Mzunguko ni Takriban Shilingi 50,000 huku Magonjwa anatakiwa kupata tiba ya Mionzi kwa mizunguko Sita ya Mionzi.

"Kumekuwa na Changamoto ya Upatikanaji wa Dawa ,Dawa za Saratani ni Ghali tunaomba SERIKALI iweze kugharimia tiba ya Satani" Amesema Mhanga huyo wa Saratani.

Naye Ostadhi Ramadhani (57) ambaye pia Ni muhanga wa Saratani Amesema Alianza Kuona Dalili za Ugonjwa huo Mwaka 2005 nakuanza tiba 2022 na kubaini kuwa Ugonjwa huo wa Saratani upo hatua ya pili ya Ugonjwa huo.

Amesema Alianza kuhudhulia Matibabu pasipo kumjulisha Mkewe na kuanza kuficha Siri Juu ya Ugonjwa huo.

"Nikaanza kutumia tiba ya Mionzi pasipo kumjulisha Mke wangu, Mionzi hii haiunguzi unajihisi Baridi chakufurahisha Watoa Huduma wanatoa Huduma kwa Usawa"Amesema Ostadhi Ramadhani.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.