TOSCI YAWAASA WAKULIMA KUJISAJILI KWENYE MFUMO WA RUZUKU YA MBEGU
Na Mwandishi wetu,TANGA
TAASISI ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI ) imeendelea kuwaasa wakulima kujisajili kwenye mfumo wa Ruzuku wa Mbegu.
Kauli hiyo imetolewa leo Octoba ,16,2025 na Mkurugenzi wa Tathimini na majaribio kutoka TOSCI Matenga M. Swai kwenye viwanja vya Usagara Jijini Tanga wakati wa kilele Cha Maadhimisho ya siku ya chakula Duniani yenye kauli mbiu ya Tuungane pamoja kupata chakula Bora kwa Maisha Bora ya Baadae.
Matenga amesema wakulima na Watanzania wote washirikiane kwa pamoja ili wapate Mbegu Bora na wazingatie Ubora kwa maana hiyo wanunue Mbegu zilizopo kwenye vifungashio na waakikishe wanapewa risti.
Amesema TOSCI imeanzisha mfumo wa usajili Mtandao yaani Online.ambao unasajili kwa mfumo wa Ruzuku kuanzia ngazi ya Wilaya
Ameongeza kuwa majukumu ya TOSCI ni kushugulikia maswala ya Mbegu kukagua maghala hayo yanafanywa kwa kushirikiana na Maafisa ugani waliopewa mafunzo na TOSCI.
Ameongeza kuwa wanapita kwa wauzaji yaani madukani Lengo ni kuona Mbegu zinanazouzwa zina ubora maana Mbegu ni kitu ambacbo Kiko hai.
kwa upande wake mnufaika wa mradi wa BBT. Ndogowe(Mama Samia Block farm) DODOMA. NduguHafidhi mambole amesema wamenufaika vitu vikuu vinne elimu, aridhi,mtaji, pamoja na Masoko
Amesema kupitia TOSCI wamenufaika kwa kupata Mbegu Bora ambazo zinaleta tija kwenye mavuno hali ambayo inapelekea kupata kipato kizuri kinachowasaidia kuendesha uchumi wao 

Comments
Post a Comment