LUFEZUWA AWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA AMANI
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Temeke kupitia chama Cha National Labour Party (TLP),Mohamed Shabani Lufezuwa amewataka watanzania kudumisha amani,kwani amani ndiyo nguzo kuu ya maendeleo ya taifa lolote duniani
Hayo ameyabainisha na mwandishi katika mahojiano maalum na mwandishi wa Dmnews Jijini Dar es Salaam amesema kwamba "niwaombe watanzania wenzangu siku zimeisha tunakaribia kwenda kupiga kura bado siku chache kwahiyo tukapige kura kwa amani na tukawachague wagombea wa TLP kwa nafasi ya Urais,Ubunge na Udiwani ili tuwaletee maendeleo watanzania
Mgombea Lufezuwa amebainisha vipaumbele kwa maendeleo ya Jimbo la Temeke ambavyo ni elimu,uchumi na huduma za jamii .
Amesema endapo atapata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo Hilo nitahakikisha kwamba uchumi unakuwa Kwa Kasi kwa wananchi wa Jimbo la Temeke
"Niwaombe sana ,Watanzania wenzangu,mkapige kura kwa amanu na kukiletea ushindi wa kishindo Chama Cha TLP",amesema Lufezuwa
Comments
Post a Comment