KIBONDE AWATAKA WATANZANIA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA OKTOBA 29

  Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

              Chato,Geita

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Makini, Coaster Kibonde amewaomba watanzania kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 ili waweze kutimiza haki Yao ya kikatiba .

Hayo ameyabainisha Oktoba 17,2025 alipotembelea nyumbani kwa Hayati John Pombe Magufuli Chato Mkoani Geita na kupata fursa ya kuzuru kaburi la hayati Magufuli.

Mgombea Kibonde ameambatana na mgombea Mweza , Azza Haji Suleiman na Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia chama cha Makini,Ameir Hasani Ameiri na viongozi wengine wa Chama akiwemo Makamu Mwenyekiti Bara,Gress Boniface Ngonyani,Katibu mwenezi Taifa Fahim Nassor na Naibu Katibu Mwenezi Taifa, Ramadhani Said Bambo pamoja na Mkuu wa Idara ya Urafiti,Sera na Nyaraka, John January Mboya mkoa wa Geita ambao ni mkoa wa 20 toka aanze kampeni za kuwaomba kura watanzania .

"Niwaombe Watanzania wenzangu tujitokeze kwa wingi tukapige kura kwa amani na kuwaasa watanzania baada ya kumaliza kupiga kura kurudi nyumbani  ili kusubiria matokeo,pia alitumia fursa hiyo kuendelea kuwaomba watanzania kutowasikiliza wanaochochea maandamano siku ya kupiga kura",amesema Kibonde

Alisisitiza kwamba Oktoba 29,2025 ni siku maalumu kwa upigaji kura na ni takwa la kisheria Kila baada ya miaka mitano hivyo kitendo chakuhamasisha maandamano siku hiyo ni sawa na uhaini.

Aliongeza kwa kuwaomba watanzania kuwapuuza wanaochochea maandamano hayo na alizitaka taasisi za majeshi  na TCRA kuwachukulia hatua Kali za kisheria wahusika wote wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii ili iwe fundisho kwa wengine.

Hata hivyo amewaomba TCRA wafute maudhui yote yanayoleta sintofahamu ili kuendeleza kudumisha amani na utulivu tuliorithi kutoka kwa waasisi wa Taifa letu.

Alimalizia kwamba amani ni Tunu ya Taifa letu tuienzi na kuidumisha kwa gharama yoyote kwa maslahi mapana ya nchi yetu "niwaombe watanzania kudumisha amani wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi",   

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA TATU WA KIMATAIFA WA WATU WENYE ULEMAVU UJERUMANI.