GEKULA:WANANCHI NICHAGUENI NIWALETEE MAENDELEO MAJOHE.
Mgombea Udiwani kata ya Majohe katikati aliyevaa shaeti la kijani Julius Gekula Warioba akiwasili katika mtaa wa rada Manispaa ya ilala . ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Octoba 29,mwaka huu nchi nzima .
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline
DAR ES SALAAM
MGOMBEA Udiwani kata ya Majohe Halmashauri ya Ilala jijini Dar es salaam Julius Gekula Warioba amewaeleza wananchi wa kata hiyo Umuhimu wa kumchagua kuwa diwani wao na kwamba akiwa katika nafasi za ujumbe wa Serikali ya mtaa na Ofisa mtendaji wa mtaa huko nyuma alifanya kazi kwa uadilifu mkubwa.
Amesema anaishukuru Chama chake Cha Mapinduzi CCM na wanaccm wa kata ya majohe kuweza kumwamini na kukubari kupeperusha bendera ya Chama kwa nafasi ya Udiwani hivyo jukumu alililonalo huko mbele baada ya kuchaguliwa Octoba 29,mwaka huu. Nikuwatumikia wananchi hao kwa uweza wake wote.
Gekula ameyasema hayo leo Octoba 16 ,2025 katika mkutano wa kampeni za Chama hicho uliofanyika katika mtaa wa rada ndani ya kata hiyo ya majohe ambapo amesema wananchi wasifanye makosa na badala yake wajitokeze kwa wingi kukichagua Chama Cha Mapinduzi CCM katika nafasi ya Urais,ubunge na Udiwani.
Akizungumzia mipango na kazi nzuri inayofanywa na Mgombea wa CCM ambaye ndio Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema katika Kata ya majohe katika kipindi Cha mwaka 2025 /30 wanatarajia kupata Barabara za lami kuzunguka mitaa mbalimbali na muda wote ujenzi unatarajia kuaza .
Amesema kata ya majohe serikali chini ya Rais Dkt. samia Suluhu Hassan imejipanga kujenga Barabara nyingi ili kurahisisha mawasiliano baina ya mitaa na mitaa Lengo likiwa ni kuchochea shughuli za Maendeleo za wananchi wa kata ya majohe na maeneo mengine .
Gekula amesema kuwa zipo Barabara zingine za changarawe ambazo nazo atakwenda kusimamia kuhakikisha zinajengwa na wananchi wanapita bila wasiwasi.
Kuhusu elimu pia amesema Mgombea urais wa a CCM Dkt Samia Suluhu Hassan ameleta fedha nyingi kujenga madarasa na miundombinu mbalimbali ya shule ili kuwezesha watoto kusoma pasipokuwa na changamoto yeyote.
Gekula amesema kutokana na kazi zote ambazo amezifanya Mgombea huyo wa Urais amewaeleza wananchi endapo watamchagua eneo hilo la Majohe A atahakikisha wanajenga zahanati.
Pia amesema Dkt samia amefanya Maendeleo mengi amejenga vituo vya afya na watajenga zahanati hapo na katika upande wa elimu watajenga shule ya Msingi na sekondari lakini ujenzi wa vivuko na madara vyote vjtajengwa ili kurahisha wananchi kupita kirahisi.
"shida ya vivuko kweneye maeneo korofi yote yatashughulikiwa kikamilifu hivyo wananchi jukumu lenu kubwa ni kuchagua Chama Cha Mapinduzi CCM Octoba 29,mwaka huu."amesema
Kuhusu Ulinzi na Usalama amesema wamejenga kituo Cha Polisi Majohe juu na jumla ya shilingi zaidi 113.zitafanya kazi ya kumalizia kituo hicho Cha Polisi hivyo jukumu lake kubwa nikwenda kusimamia ili kuweza kukamilika kwa kituo hicho.
Amesema hakuna Maendeleo pasipokuwa na amani hivyo amewaasa wananchi waache mara Moja ndoto ya kutaka kufanya maandamano badala yake wanatakiwa kwenda kupiga kura na kurudi nyumbani.
" Wanaotaka kuandamana wanatakiwa kuulizwa watoto wao wako wapi na wanasoma wapi na kuirudisha amani mahala ambapo penye machafuko ni kazi kubwa sana "amesema
katika hatua nyingine amesema akichaguliwa tu anakwenda kusukuma ujenzi wa ofisi za serikali ya mtaa ili wananchi waweze kupata huduma pasipokuwa na changamoto zozote
Amewaeleza wananchi kuwa yeye akichaguliwa huduma zote za serikali ya mtaa ni bure na mwananchi yeyote ambaye atadaiwa fedha basi atoe taarifa kwake.
Naye Mwenyekiti CCM kata ya majohe Nuru Mizumo amewataka wanachama wa Chama hicho kuwa wasidanganyike badala yake wampe kura za kutosha Julius Mataro Gekula .
Amesema Mgombea huyo hana shida na na sio kiongozi yule wakujilimbikizia Mali yeye anajitosheleza yeye amekuja kusaidia wananchi wa kata hiyo ya majohe .
Amesema jambo kubwa la wanaccm na wananchi kwa ujumla ni kuchagua mafiga matatu ambapo wachague rais anayetokana na Chama Cha Mapinduzi CCM.
Kwaupande wake mgeni mwalikwa Florian Karugaba ambaye alikuwa Mgombea ubunge kivule akizungumza katika mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika mtaa wa rada.
Karugaba amesema Rais .Dkt. Samia anatafufa maendeleo na wananchi wasije kudanganyika kwani kiongozi huyo anamalengo makubwa sana kwa Maendeleo ya wananchi wake.
Amesema Dkt. Samia ameleta Urais wa vijana kwenda veta kwani mtoto akimaliza anakwenda veta kupata ujuzi huyo ndio Dkt.samia Suluhu Hassan. 

Comments
Post a Comment