ULEGA: KATIBA MPYA UHAKIKA KWA DKT SAMIA
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline
MKURANGA
MGOMBEA ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Jimbo la mkuranga Alhaj Abdallah Ulega amewataka watanzania kama wanataka katiba mpya basi wanapaswa kumchagua Dkt Samia Suluhu Hassan kwani yeye alikuwepo katika machakato wa katiba .
Amesema hata katika uzinduzi wa kampeni kitaifa zilizofanyika jijini Dar es salaam Agost 27,2025 katika Viwanja vya Tanganyika perkas amesema ametamka kuwa katika siku 100 za mwanzo atahakikisha anafufua mpya mchakato wa katiba mpya.
Ulega amesema maneno haya leo Septemba 6,2025 katika uzinduzi wa kampeni Jimbo la mkuranga ambapo amesema Dkt .Samia ni muumini wa mariadhiano na akitamka anatenda huyo ndio daktari Samia .
Amesema kuwa jambo Moja tu kwa watanzania na wananchi wa Jimbo la mkuranga ni kuhakikisha wanampigia kura za kutosha mgombea wa Chama Cha Mapinduzi CCM ili aweze kutimiza mambo makubwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi .
Pia Ulega amezungumzia Barabara ya kilwa kutoka mbagala rangi tatu hadi kongowe kutanuliwa ili kurahisisha usafiri katika eneo hilo na Juhudi za kufanya kazi hiyo ndio zimeaza.
Waziri ulega akizungumza na wananchi hao wakati akizungumzia Maendeleo na mambo mbalimbali ambayo yamefanyika katika Jimbo la mkuranga amesema wananchi hao wakimpa kura za kutosha na yeye wakimchagua atakwenda kumuomba mama ili kuweza kupandisha hadhi wilaya ya mkuranga na kuwa Halmashauri ya Manispaa ya mkuranga .
Amesema wilaya hiyo inastahili kuwa Manispaa kutokana na uwepo wa viwanda vya kutosha katika Jimbo hilo ambapo amesema hivi sasa wilaya hiyo inaviwanda vidogo zaidi ya 100 na viwanda vikubwa zaidi 70 hivyo inastahili mkuranga kuwa Manispaa
Ameongoza kuwa leo umezinduliwa mkutano wa kampeni na yeye na madiwani wake watafanya kampeni za Kistarabu na wanakwenda kata kwa kata ili kumuombea kura Dkt.samia Suluhu Hassan ili kuhakikisha wanapata kura nyingi.
Mgombea huyo pia aliwaeleza wananchi hao kuwa amani ya Taifa ndio inayofanya wajadili viwanda ,na mahala ambapo hakuna amani huwezi Kujadili maji,viwanda ,Barabara,ajira ,na mambo mengine huku akiwaomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa .
Amesema kutokana na amani iliyopo leo hii mkristo na muislamu wanaishi nyumba Moja na kupeana hata chakula hilo ni Somo tosha la uwepo wa amani .
Katika uzinduzi wa kampeni hizo pia wananchi kutoka katika vyama vingine vya upinzani ikiwemo wa chama Cha wananchi CUF na wengine kutoka Chama Cha Act _Wazalendo wapato 89 wametangaza kurudi Chama Cha Mapinduzi CCM huku wakiandika ujumbe wa 'TUNARUDI KWA MAMA' 

Comments
Post a Comment