TLP KUTOA MWAROBAINI WA AJIRA KWA VIJANA
Timothy Marko,DmNews online
DAR ES SALAAM
WAKATI kampeni za uchaguzi zikiwa tayari zimeshaaza Kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Octoba 29 mwaka huu Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Tanzania Labor party (TLP)Rwamugira Yustas amesema kama atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania atawakopesha Vijana na Wanawake Matrekta madogo madogo ili kuweza kuboresha hali zao kiuchumi kupitia Sekta ya Kilimo.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Rwamugira Yustas amesema kuwa watanzania wakimpa ridhaa kuwa Rais atahakikisha wakulima Nchini wanapewa pembe jeo zitakazo ratidiwa na wakuu wa Mikoa na Wilaya.
"Hatutaki Mlolongo wa kupata pembejeo , Sambamba na hilo tutaboresha Sekta ya Viwanda Vidogo ili Vijana waweza kupata Ajira."Yustas.
Ameongeza kuwa ilani ya Chama hicho itawawezesha kupata Mashine za kuunganisha Vyuma ilikuweza kuchochea Sekta ya Viwanda.
"Nikipewa Ridhaa na Wananchi Nitahakikisha Vijana wanapatiwa Mikopo na fuu isiyo nariba ili kuweza kuzalisha "Amesisitiza Yustas.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Taifa kupitia Chama hicho, Richard Lyimo amesema yeye kwa wadhifa ni mwenyekiti wa Chama hicho lakini Amepisha Rwamugira Yustas ambaye ni katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labor party (TLP).
Amesema kuwa hana shaka nauwezo wa Mgombea huyo kwani n mchapa kazi.
"Tumemkabidhi Sera ya Chama ambacho kipaumbele chake ni Kudumisha Amani,Huwezi Kudumisha Uchumi pasipokuwa na taifa lenye Amani"Lyimo.
Lyimo Ameongeza kuwa katika Kuwania kiti cha Urais atahakikisha Amani inakuwa kipaumbele cha Chama hicho nakusisitiza hawato penda kupata Majeraha Mara baada ya Uchaguzi kukamilika.
"Mgombea Wetu mpeni kura za ndio nitapambana kutatua Changamoto za Usafiri kwa Wanafunzi"Amebainisha Lyimo.
Aidha, Makamu Mwenyekiti Taifa wa Tanzania Labor party (TLP) Johari Rashid amesema atahakikisha kero ya Upatikanaji wa Bima ya Afya inakwenda kupata majibu
Amesema Kumekuwa na Changamoto za Upatikanaji wa Bima kwa kundi la Wazee na Vijana."Bima ya Afya imekuwa Changamoto sio kwa Wazee bali hata Vijana"Amesema Johari Rashid .
Comments
Post a Comment