SUFIAN MGUDE: APONGEZWA NA WANANCHI KATA YA MSEKE_ TANANGOZI IRINGA.

Na  Eliasa Ally ,DmNewsonline 

                IRINGA 

WANANCHI wa Kata ya Mseke Tanangozi Mkoani Iringa wamemshukuru na kumpongeza mdau wa Maendeleo Sufian Mgude kwa kujitokeza kujenga kituo Cha Polisi ndani ya kata hiyo nakubainisha kuwa kituo hicho kinakwenda kutibu changamoto mbalimbali zilizokuwa zinajitokeza kwa wananchi.

Wamesema kata hiyo ambayo pia inapita Barabara kubwa ya kutoka Dar es salaam awali kulikuwa na changamoto nyingi ikiwamo uwizi wa mafuta kwenye magari, ajali za barabarani lakini kitendo Cha mdau huyo kujenga kituo ambacho sasa askari wanakuwepo kumeleta faraja na Usalama kwa wananchi wanauzunguka eneo hilo.

Wakizungumza katika mahojiano maalumu na Mwandishi wa habari hizi kutoka mkoani Iringa mapema mwezi huu ,Pius kadinde amesema kuwa wanamshukuru sana ndugu Sufian Mgude kwani amekwenda kuondoa masuala mazima ya uhalifu na zaidi kupunguza ajali za barabarani kwani awali ajali za barabarani zilikuwa nyingi na watu walikuwa wanagongwa sana magari.

"Kwakweli sisi kama wananchi wa Mseke tunamshukuru sana  Mgude ametufanya sasa tufanye shughuli zetu kwa Usalama zaidi kitendo cha kujenga kituo Cha Polisi kwenye eneo hili kumeleta Usalama sana ,kama.mnavyoona hapa kituo kizuri kikubwa sasa Polisi watakuwepo hapa kuaza askari wa usalama barabarani hadi askari wakawaida."amesema 

Kwaupande wake ratifa daud amesema kabla ya uwepo wa hicho kituo vitendo vya uhalifu vilikuwepo lakini sasa tunalishukuru Jeshi la Polisi chini ya mkuu wa mkoa wa Iringa Kheri James kwa ushirikiano mkubwa wa Sufian Mgude kwa kuleta kituo Cha Polisi katika Kata ya Mseke.

Amefafanua kuwa awali katika eneo hilo la Tanangozi hata gari zikiharibika wezi wa mafuta walikuwa wengi lakini mbaya zaidi ajali za barabarani zilikuwa nyingi sana watu wengi wamegongwa na kupoteza maisha kutokana  na kukosekana kituo Cha Polisi lakini kwasasa Imani yao kituo kimekwenda kutibu changamoto zilizokuwepo awali

Kwaupande wake mdau huyo wa Maendeleo Sufian Mgude amesema yeye kazi yake kubwa kama mtanzania ni kuhakikisha anaunga mkono Juhudi za Serikali za kuwaletea Maendeleo wananchi wake.

Ametolea mfano kata Mseke eneo hilo la tanangozo amesema kuwa wananchi walikuwa wanapata shida kufikia huduma muhimu hususani jambo ambalo lilikuwa kinahusu Polisi lakini pia uhalifu ulikuwa mwingi na ndio maana ameguswa na kuamua kujenga kituo Cha Polisi ambacho ameshakabidhi kwa serikaii.

Amesema kiu yake nikuona akina mama na wananchi kwa ujumla wanafanya shughuli zao pasipokuwa na mashaka Wala hofu kwa sababu tayari Jeshi la Polisi lipo hapo kitu kikubwa wananchi waendelea kutoa ushirikiano.

Amefafanua kuwa  yeye kama mdau wa Maendeleo kazi yake kubwa nikuunga mkono Juhudi na tayari ameshafanya mambo mengi ikiwemo ujenzi wa miundombinu mingine mingi tu ndani ya mkoa wa Iringa na mahala pengine .   

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025