SERIKALI YAWATAKA VIJANA KUCHANGAMKIA UFUGAJI WA NGURUWE.
TimothyMarko, DmNewsonline .
DAR ES SALAAM
SERIKALI imewataka Vijana kukukimbilia fursa ya Ufugaji wa Nguruwe ilikuweza kujipatia kipato kitakacho wakwamua kiuchumi.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo na Uvuvi Agnes Meena Jijini Dar es Salaam kwenye kongamano la Kimataifa la fursa za ufugaji wa Nguruwe Barani Afrika (The Africa international Pig conference Expo 2025)
Amesema kuwa Sekta ya Nguruwe imekuwa ikuwa kwa Kasi Ambapo Tanzania inakadiriwa kuwa na Nguruwe milioni 4.1 na kusababisha ajira kwa vijana
"Pamoja na ukuwaji wa Sekta hii ,Sekta hii ya Ufugaji wa Nguruwe inakabiliwa na Changamoto ya homa ya Nguruwe, Ukosefu wa Masoko kutoka Nje,"Amesema Katibu Mkuu wa wizara ya Mifugo Agnes Meena.
Meena ameongeza kuwa Pamoja na kuwepo kwa Changamoto hizo serikali imejipanga kuimarisha Sekta hiyo .
Amesisitiza kuwa Nivyema wadau wa Sekta binafsi kuweza kushirikiana serikali ili kuwekeza Sekta hiyo.
Naye Mkurugezi wa Taasisi ya Wafugaji wa Nguruwe Nchini Nigeria Profesa Adesehinwa amesema Nivyema Africa wakaungana ili kuweza kukuza Biashara na kuweza kukuza Uchumi ikiwemo ukuwaji wa Sekta ya ufugaji wa Nguruwe.
Amesema kuwa Nchini Nigeria Sekta ya Ufugaji wa Nguruwe imekuwa ikichangia Uchumi wa Nchi hiyo.
"Nyama ya Nguruwe imekuwa ikichangia Ukuwaji wa Uchumi wa Barani Africa"Amesema Profesa Adesehinwa.
Aidha, Mwenyekiti wa Wafugaji wa Nguruwe Nchini Tanzania (TAPIFA) Doreen Maro Amesema kuwa kongamano Hilo linalojumuisha Nchi za Nigeria, Afrika kusini, Tanzania.
Amesema Nchi ya Tanzania imepewa heshima kubwa kuwa mwenyeji wa kongamano la Wafugaji wa Nguruwe Barani Afrika.
"Sekta ya Ufugaji wa Nguruwe imekuwa ikikuwa kwa Kasi Nchini Tanzania Tangu 2020"Amesema Mwenyekiti TAPIFA Doreen Maro.
Comments
Post a Comment