RIDHIWANI KIKWETE :MKURANGA KUNA MABADILIKO MAKUBWA
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline
MKURANGA
MBUNGE mteule wa Jimbo la chalinze mkoani Pwani Ridhiwani kikwete amewataka wananchi wa Jimbo la mkuranga kuhakikisha hawafanyi makosa na wamchagua Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgombea ubunge wa Jimbo la mkuranga Alhaj Abdallah Hamis Ulega kwani kazi kubwa imefanyika katika kipindi chao.
Amesema kuwa mkuranga ya wakati huo sio mkuranga ya sasa kwani hivi sasa mkuranga inang'ara na maendeleo yanaonekana na hiyo nikutokana na kazi kubwa iliyofanyika na Alhaj Ulega ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi anaeshughulika na Ujenzi wa Barabara hapa Nchini.
Ridhiwani ameyasema hayo leo Septemba ,2025 katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Rais,Ubunge,na Madiwani.ambapo amesema kuwa Ulega ni mtu wa watu na ndio maana kupitia uchapakazi wake akaonekana na kuteuliwa kuwa Naibu waziri kwa wizara mbalimbali na kwasasa ndio waziri wa Ujenzi.
Akizungumzia mahusiano yake na Abdallah Ulega amesema wameaza kujuana miaka mingi tangu wakiwa vijana wadogo kwa kutokea vyuoni na mwisho wa siku wakajikuta wakitamani kuingia kwenye siasa.
Amesema kuwa wakati Abdallah Ulega akiwa mwenyekiti wa vijana mkoa Pwani yeye alikuwa Mjumbe wake hivyo kwakifupi kiongozi huyo anafanya kazi kubwa na yakuonekana na ifikapo octobar 29 mwaka huu wahakikishe wanapiga kura nyingi kwa Mbunge huyo na kura za kutosha kwa mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi CCM
Kwaupande wake Mgombea ubunge wa Jimbo la kibaha vijijini Hamoud Jumaa ambaye naye alikuwepo kwenye uzinduzi huo amesema kuwa Rais .Dkt.Samia katika kipindi Chake Cha uongozi wake amefanya kazi kubwa sana wa ujenzi wa nchi yetu.
Amesema kutokana na kazi hiyo kubwa ambayo amefanya akisaidiwa na wasaidizi wake akiwemo Mgombea ubunge wa Jimbo hilo ambaye hivi sasa ndio waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega wamefanya kazi kubwa kwa Maendeleo ya Tanzania
"Otobar 29, mwaka huu kwa pamoja nawaomba sana wananchi wa Jimbo la mkuranga nendeni mkapige kura za ndio kwa wagombea wa CCM .ili kukifanya Chama hicho kushinda kwa kishindo ."amesema Jumaa.
Mbali na viongozi hao pia uzinduzi huo umehudhuliwa na viongozi wengine mbalimbali kutoka mkoa wa Pwani wakiongozwa na mgeni rasmi UWT CCM Taifa Mary Chatanda na Mwenyekiti mstaafu wa Umoja huo Sophia Simba. 

Comments
Post a Comment