REVIVE HOSPITALI KUTOA MATIBABU BURE SEPTEMBA 6 JIJINI DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
TAASISIi ya Rivaivu(Revive) iliopo Jijini Dar s Salaam jirani na hospitali ya Ocean Road inatarajiwa kutoa huduma za matibabu bure bila malipo Septemba 6 na 7 ,2025 ikiwa ni maadhimisho ya siku ya kimataifa ya matibabu ya Physiotherapy.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji na muasisi wa Taasisi hiyo ya Revive Dkt.Lekhani Pashine amesema wameamua kuadhimisha siku hiyo kwa kutoa huduma za matibabu ya Physiotherapy ili kuongeza uelewa wa tiba hiyo kwa jamii huku mmoja wa wataalamu wa tiba hiyo Nathanaeli Stanley
Akizungumza jijini Dar es salaam na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji na Muasisi wa Taasisi hiyo ya Revive Dokta Lekhani Pashine amesema wameamua kuadhimisha siku hiyo kwa kutoa huduma za matibabu ya Physiotherapy ili kuongeza uelewa wa tiba hiyo kwa jamii huku mmoja wa wataalamu wa tiba hiyo Nathanaeli Stanley akifafanua kuhusu huduma hiyo na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma
Hata hivyo Mtaalamu huyo wa matibabu ya Physiotherapy Nathanael Stanley ametumia mchoro wa uti wa mgongo wa binadamu kueleza maradhi ya maumivu ya viungo na tatizo la ganzi miguuni linavyotokea na matibabu hayo yalivyo.
Naye Mtaalamu wa
Physiotherapy kwa watoto ,Dianarose Mtery akiwataka wazazi wenye watoto wenye utindio kujitokeza kwa wingi
Maadhimisho ya siku ya kimataifa ya matibabu ya Physiotherapy yanatarajia kufanyika Septemba 8 mwaka huu siku ya jumatatu lakini hospitali ya Revive wameamua kufanya maadhimisho hayo siku za mwisho wa wiki ili kuhudumia watu wakiwa mapumziko ambapo huduma zitafanyika kwenye kituo kilichopo Posta jirani na Hospitali ya Ocean 

Comments
Post a Comment