NORWAY NA HLRC WAINGIA MAKUBALIANO KATIKA KUKUZA DEMOKRASIA NCHINI.
Timothy Marko DmNews online
DAR ES SALAAM
KITUO cha Haki za binadamu Nchini LHRC kimeingia Makubaliano na Ubalozi wa Norway kuimarisha msaada wa kisheria, Haki jinai na kuimarisha wa Utawala Bora.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugezi wa Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu Nchini LHRC Fulafulue Masawe amesema kuwa Mkataba huo Wenye thamani ya Sh. bilioni 61.9 unalenga kukuza Haki za Bindamu Nchini.
"Nchi ya Norway imekuwa mdau Muhimu wa ukuzaji wa Demokrasia Nchini na Haki za binadamu na kukuza Misingi ya Utawala Bora Nchini"Amesema Masawe.
Masawe Ameongeza kuwa Nchi ya Norway pia imekuwa mstari wa mbele katika Masuala Haki jinai, Mchakato wa Uchaguzi,Utetezi wa Haki za makundi Maalum ikiwemo Wanawake na watoto.
Kwaupande wake Balozi wa Norway Nchini Tanzania Tone Tinnes amesema Mkataba huo unalenga kukuza Msaada wa kisheria, Demokrasia na Haki za Bindamu.
Amesema Norway Imekuwa mdau Muhimu wa Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu Nchini LHRC Tangu 2013.
"Lengo letu nikuweza kukuza Uelewa wa Masuala Haki za Kisiasa, Uwezeshwaji wa wa Wanawake kiuchumi,na kukuza Uhuru wa kujieleza " Amesema Balozi wa Norway Tone Tinnes.
Balozi Tinnes Ameongeza kuwa Asasi za kirahia zinazomchango wa kukuza Demokrasia Nchini.
"Maridhiano ndio Msingi wa kukuza Demokrasia Nchini na kukuza Misingi ya kujieleza "
Comments
Post a Comment