NJAMA AAHIDI MAKUBWA KOROGWE NDANI YA SIKU 100 AKIPATA RIDHAA YA WANANCHI

Mgombea Mwenza wa urais Balozi              Dkt. Nchimbi (kushoto) akimnadiCPA Njama.




Na Yusuph Mussa,DmNewsonline

                           Korogwe

MGOMBEA ubunge Jimbo la Korogwe Mjini mkoani Tanga CPA Charles Njama ameahidi makubwa ndani ya siku 100 za uongozi wake kwa kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Miji 28, na Mradi wa Maji kwa kutumia chanzo cha Mto Ndemaha itakuwa imekamilika, na wananchi wa Korogwe shida ya maji itabaki historia kwao.

Pia,  barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami kutoka barabara kuu hadi Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Magunga yenye kilomita 2.7, na ile ya kutoka Kibo, Mtonga- Mgombezi- Bagamoyo, njiapanda ya Handeni yenye urefu wa kilomita 6.7, ndani ya siku 100 za uongozi wake, Mkandarasi atakuwa kazini.

Ameyasema hayo Septemba 15, 2025 mbele ya Mgombea Mwenza kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sokoni mjini Korogwe.

"Korogwe Mjini kuna miradi mikubwa ya maji inakwenda kutekelezwa. Kuna Mradi wa Maji wa Miji 28, na kuna Mradi wa Maji wenye chanzo kutoka Mto Ndemaha, hii yote inakwenda kukamilika ndani ya muda mfupi ujao. Na mimi naahidi kwenu, ndani ya siku zangu 100 za kwanza, mradi huu unakwenda kukamilika, na Korogwe hatutakuwa na shida ya maji tena.

"Tunayo barabara yetu ya kutoka NMB kwenda Magunga. Barabara hii mnaiona hali iliyokuwa nayo, lakini tumepata fungu (fedha), hivyo tunakwenda kuitengeneza kwa kiwango cha lami na kuweka taa za barabarani na mifereji, ambayo inaenda kuanza mapema iwezekanavyo. Niwaahidi, ndani ya siku 100 za uongozi wangu, mtamuona Mkandarasi anafanya kazi, na nitashirikiana na Serikali yangu kuona mkandarasi anafanya kazi na kukamilisha kwa wakati. Vile vile kuna barabara ya kutoka Mtonga- Mgombezi hadi Bagamoyo, nayo inajengwa kwa kiwango cha lami, kuwekwa taa na mifereji" amesema Njama.

Njama amesema Ilani ya CCM kwa mwaka 2025- 2030 imesheheni mambo mengi kwa ajili ya miradi mbalimbali kwa wananchi wa Jimbo lacKorogwe Mjini ikiwemo elimu, afya, maji, barabara, kilimo na uvuvi, lakini amebahatika kukaa na vikundi mbalimbali kuanzia wajane na akina Mamalishe na babalishe, vikundi vya bodaboda, bajaj na maguta. Sokoni amekutana na wanawake wanaouza mahindi na mbogamboga, na kubainisha makundi hayo ni muhimu sana kwake.

"Baada ya kuteuliwa ninefanya vikao vya ndani na makundi mbalimbali, nimekaa na akina Mamalishe na babalishe, wajane, nimekaa na vikundi vya bodaboda, bajaj na maguta. Nimepita sokoni na kukutana na wanawake wanaouza mahindi na mbogamboga, na wafanyabiashara wadogo. wote hao nimewasikiliza, na nimegundua changamoto ambazo tunakwenda kuzitatua. 

"Ndani ya siku 100 za kwanza,  nitahakikisha tunakwenda kuanzisha vikundi ambavyo vitakuwa na akaunti benki, na utaratibu wa kuchangia kidogo ili viwe tayari kupokea uwezeshwaji wa kiuchumi. Hilo tayari tunakwenda kufanya kwa pamoja, na tunakwenda kubadilisha uchumi wetu, na kuibadilisha Korogwe yetu" CPA Njama. 
  


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025