MSAMA :MAPOKEZI ANAYOPATA MGOMBEA URAIS CCM DKT SAMIA NI ISHARA NZURI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025.
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline
DAR ES SALAAM
MKURUGENZI wa Msama Promotions, Alex Msama, ametoa pongezi zake kwa Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha ukakamavu wa hali ya juu tangu alipoaza kampeni Agosti 28,2025.
Msama amesema katika kampeni alizozifanya kwa wiki kadhaa sasa tena pasipo kupumzika ni kielelezo kikubwa cha ukakamavu na dhamira ya kweli ya kuwatumikia Watanzania.
Kauli hiyo ametoa jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na Waandishi wa habari akizungumzia tathimini yake ya tangu Mgombea huyo Urais kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan aaze ziara zake hizo za kampeni ,ambapo Msama amebainisha kuwa mapokezi makubwa anayoyapata Dkt. Samia ni dalili tosha za ushindi mkubwa unaomsubiri katika uchaguzi ujao.
Pia amewataka watu wanaoendeleza lugha za matusi mitandaoni kuacha mara moja, nakudai watanzania wasipoteze muda kuwajibu bali wawapuuze kwani wengi wao wanatumiwa na nguvu za kigeni zisizo na nia njema kwa Taifa.
Comments
Post a Comment