MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA TEMEKE AAHIDI UJENZI WA KITUO CHA KISASA STENDI YA DALADALA TEMEKE MWISHO

Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

             DAR ES SALAAM 

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Temeke kupitia  Chama Cha Wakulima(AAFP),Yusuph Rai amesema kwamba endapo atapata ridhaa ya kuwa Mbunge katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025 atahakikisha Temeke Mwisho kunajengwa kituo kikubwa Cha daladala chenye hadhi na thamani ya Wilaya ya Temeke pamoja na  kituo kitakachounganisha magari yanayokwenda Mikoa ya  Kusini ili kuongeza thamanj ya mapato ya Jimbo  Hilo.


Amezungumza hayo leo Septemba 15,2025 katika uzinduzi wa kampeni za Jimbo la Temeke zilizofanyika katika Viwanja vya Tandika Sokoni kata ya Tandika Jijini Dar es Salaam.

Aidha ,amesema kwamba soko la Tandika ndio kariakoo ya Temeke,hivyo akipata nafasi ya kuwa mbunge atahakikisha soko hilo kuwa kubwa na liwe la kimataifa pamoja na kuishawishi serikali ili Soko hilo liwe kitovu cha biashara.

Pia amesema kwamba Tandika imekuwa na changamoto ya maji safi na salama  kwa siku nyingi kwahiyo nitahakikisha uchimbaji wa visima kwa kila mtaa  ili wananchi wapate maji safi na salama

Hata hivyo ,amesema hali ya uzoaji takataka kwa eneo la Tandika kumekuwa na tatizo la wakandarasi kuzoa takataka kwa kusuasua kutokana na vitendea kazi duni hivyo kusababisha takataka kuzolewa kwa muda mrefu huku zikisababisha mlipuko wa magonjwa mbalimbali na kusababisha kero ya harufu mbaya kwa hiyo nikipata nafasi ya kuwa mbunge nitahakikisha  kutumia pesa za mfuko wa Jimbo ili kila  kata ipate gari moja kwa ajili ya kuzoa takataka kwa kata zote
 
Sanjari na hayo katika elimu atahakikisha ana boresha miundombinu kuwa ya kisasa kwa kujenga majengo ya kisasa ambayo yatatumia eneo dogo na yatakayochukua wanafunzi wengi pamoja na kuhakikisha wanafunzi huwachangishwi michango kwa kuwa serikali imetuambia elimu Bure ,nitasimamia ufaulu wa wanafunzi kwani Temeke iko nyuma kwenye ufaulu.


Sambamba na hayo,Rai amesema atawekeza katika ulinzi shirikishi kwa kujenga ofisi za kisasa na kuboresha maslahi ya walinzi wa jamii ili kuhakikisha wananchi na mali zao wanalindwa dhidi ya vitendo vya kihalifu.

“Mimi ndiye mgombea ubunge kijana zaidi kwenye Jimbo la Temeke. Mkinichagua, mmechagua maendeleo, kwani nina nguvu kubwa za kuwatumikia Wanatemeke,” amesema

Kwa upande wake Katibu Itikadi na uenezi, Rashid Maokolo ameibua sakata la ujenzi wa fremu za biashara kujengwa katika hifadhi ya Barabara Mbagala amelaani suala Hilo hivyo amewataka wananchi wasipoteze kura kwa wengine nakuwataka wamchague Mgombea wa AAFP .

Naye Mgombea Udiwani Kata ya Tandika Kibuda ameahidi  kushughulika na changamoto za wafanyabiashara wa soko la Tandika kuboresha miundombinu ya kisasa pamoja na kuhakikisha mikopo ya asilimia 10 ya  akina mama na vijana inayotolewa na Halmashauri inapatikana kwa urahisi bila vikwazo vyovyote

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025