JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU MAGARI YENYE NAMBA SSH 2025
TimothyMarko ,DmNews online .
DAR ES SALAAM
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watu kumi (10)Wenye Magari yenye Namba za Usajili wa SSH 2025 nakusisitiza kuwa Magari hayo yenye Namba hizo yamekiuka sheria za usajili.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Jumanne Murillo amesema kuwa Magari hayo yamekiuka sheria 13(1) ya Sheria za Usalama Barabarani ya Mwaka 1973 na Marekebisho yake Mwaka 2023.
Pia Kamanda Murillo amesema ambamba nwanamshikilia Ashir Ashir, Nicolas Nicolas kwa tuhuma za Ulawiti Sambamba na mtu huyo pia wanamshikilia Thomas (30), Mkazi wa kivule kwa Tuhuma za kubaka
Aidha Murillo Ameongeza kuwa Mnamo Agosti 12 Jeshi hilo liliwashikilia Hassan Hamisi Mkazi wa Tandale na Elia Mapande Mkazi wa Goba kwa kosa lakujihusisha na Mtandao wa wizi wa pikipiki go Gift Shaban, Hussein Ally,Riziki Ramadhani wakazi wa Mazense kwa tuhuma za wizi wa Runinga na Simu na mkononi. 

Comments
Post a Comment