COASTER KIBONDE AKIDHI VIGEZO,CHAMA CHA MAKINI CHAWASHUKURU WANANCHI
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
CHAMA cha Makini kinapenda kutoa shukrani za dhati kwa wananchi wote waliojitokeza kwa wingi katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani kwa ajili ya kumdhamini Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chetu.
Zoezi la upatikanaji wa wadhamini lilianza rasmu tarehe 11 Agosti 2025,.mara baada ya Mheshimiwa Coaster Kibonde,Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Makini kuchukua fomu ya uteuzi.Zoezi hili limehitimishwa rasmi,tarehe 20 Agosti 2025 katika Mkoa wa Morogoro na kufuatiwa na kiapo Cha Mgombea huyo katika Mahakama Kuu ya Tanzania,hatua muhimu inayomwezesha sasa kukidhi vigezo vya kuendelea na mchakato wa uteuzi.
Mgombea wetu anatarajia kurudisha fomu ya uteuzi rasmi tarehe 27 Agosti 2025 saa 3:30 asubuhi ,Jijini Dodoma na Kisha kusubiri uamuzi na uteuzi rasmi kutoka Tume Huru ya Uchaguzi.
Tunatambua kwa dhati na kuthamini moyo wa uzalendo,mshikamano na Imani mlionyesha katika hatua hii muhimu ya kisiasa kwa chama chetu na kwa taifa kwa ujumla.Chama Cha Makini itaendelea kusimama imara kwa ajili ya maslahi ya wananchina kwa maendeleo ya kweli ya Tanzania 

Comments
Post a Comment