WATIA NIA 84 WARUDISHA FOMU ZA UBUNGE WILAYA ILALA
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
WAGOMBEA 84 waliochukua fomu za kutia nia katika nafasi ya Ubunge wamerejesha fomu za Ubunge Wilaya ya Ilala katika majimbo manne ambayo ni Ilala,Segerea,Ukonga na Kivule.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Julai 2,2025 Jijini Dar es Salaam Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Chief Sylvester Yaredi amesema mchakato wa kuchukua fomu na kurudisha fomu dirisha limefungwa saa kumi kamili .
Aidha, amesema kwamba katika zoezi hilo wagombea 87 waliochukua fomu na Wagombea 84 ndio waliorudisha fomu.
Katibu wa wilaya Yared alisema katika jimbo la Kivule wamechukua fomu 46 wamerejesha 44,Jimbo la Segerea wamechukua 18,wamerejesha 17,Jimbo la ukonga wamechukua 11 na wamerejesha 11,na Jimbo la Ilala wamechukua 12 na wamerejesha 12. 

Comments
Post a Comment