TIRDO YAJA KIVINGINE MAONESHO YA SABASABA

Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

     DAR ES SALAAM 

SHIRIKA  la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) wamewataka wananchi kutembelea Banda lao katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara(SABASABA) yanaoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Jijini Dar es Salaam .

Hayo yamebainishwa leo Julai 3,2023 na Mtaalam wa Nishati ,Ali Moh'd Rashid wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kwamba wamekuja na tafiti mbali  mojawapo ni utaalam juu ya matumizi bora ya nishati . 
 
Amesema kuwa matumizi bora ya nishati ni kutumia nishati kwa namna ambayo inapunguza upotevu wa nishati na kufikia matokeo sawa na bora bila kuathiri utendaji.

Aidha ,ameeleza kwamba inapaswa kufanya ukaguzi wa mifumo ya nishati Kila baada ya muda ili kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.

Pia,amesema kwamba kutumia vifaa vinavyotumia teknolojia za kisasa ambazo zinatumia nishati kwa ufanisi mfano Taa za LED.

Sanjarari na hayo, Mtaalamu Rashid ameendelea kwa kusema kwamba matumizi ya vyanzo vya nishati mbadala ikiwemo jua,upepo kwa kupunguza gharama.

"Kupunguza matumizi ya nishati,biashara na mashirika yanaweza kupunguza bili zao za nishati na gharama za uendeshaji",alisema

Amebainisha pia maeneo ya upotevu wa nishati na kutoa mapendekezo ya kuboresha kunaweza kusababisha uokoaji mkubwa wa nishati.

Aliendelea kwamba kuboresha utendaji wa vifaa kwa kufanya ukaguzi kutasidia kutambua mahitaji ya matengenezo na kuboresha utendaji kazi wa kifaa.

Alimalizia kwamba kuna faida kwa mzalishaji wa nishati mfano Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) huduma ya nishati inaweza kuwafikia watumiaji wengi kuwa na matumizi bora ya nishati.

MSIMU HUU WA MAONESHO YA SABASABA

Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

           DAR ES SALAAM 

SHIRIKA  la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) wamewataka wananchi kutembelea Banda lao katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara(SABASABA) yanaoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere  Jijini Dar es Salaam .

Hayo yamebainishwa leo Julai 3,2023 na Mtaalam wa Nishati ,Ali Moh'd Rashid wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kwamba wamekuja na tafiti mbali  mojawapo ni utaalam juu ya matumizi bora ya nishati . 
 
Amesema kuwa matumizi bora ya nishati ni kutumia nishati kwa namna ambayo inapunguza upotevu wa nishati na kufikia matokeo sawa na bora bila kuathiri utendaji.

Aidha ,ameeleza kwamba inapaswa kufanya ukaguzi wa mifumo ya nishati Kila baada ya muda ili kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.

Pia,amesema kwamba kutumia vifaa vinavyotumia teknolojia za kisasa ambazo zinatumia nishati kwa ufanisi mfano Taa za LED.

Sanjarari na hayo, Mtaalamu Rashid ameendelea kwa kusema kwamba matumizi ya vyanzo vya nishati mbadala ikiwemo jua,upepo kwa kupunguza gharama.

"Kupunguza matumizi ya nishati,biashara na mashirika yanaweza kupunguza bili zao za nishati na gharama za uendeshaji",alisema

Amebainisha pia maeneo ya upotevu wa nishati na kutoa mapendekezo ya kuboresha kunaweza kusababisha uokoaji mkubwa wa nishati.

Aliendelea kwamba kuboresha utendaji wa vifaa kwa kufanya ukaguzi kutasidia kutambua mahitaji ya matengenezo na kuboresha utendaji kazi wa kifaa.

Alimalizia kwamba kuna faida kwa mzalishaji wa nishati mfano Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) huduma ya nishati inaweza kuwafikia watumiaji wengi kuwa na matumizi bora ya nishati

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025