TAWA YAWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO KATIKA MAONESHO YA SABASABA
Na Angelina Mganga,DmNewsOnline
DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Wanyamapori Tanzania(TAWA) inawakaribisha watanzania kutembelea Banda lao katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara(SABASABA) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K.Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamebainishwa Leo Julai 3,2025 na Afisa Muhifadhi TAWA,
Dkt. Gladstone Mlay wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Banda la TAWA amesema kwamba kwa mwaka 2024 jumla ya watalii Milioni 5.3 wametembea hifadhi za Taifa ambapo watalii wa ndani milioni 3.2 na watilii wa Kimataifa milioni 2.1 wamepita katika maeneo mbalimbali yanayosimamiwa na Mamlaka hiyo.
Aidha ,Afisa Muhifadhi Mlay ameeleza kwamba TAWA imekusanya shilongi bilioni 3.9 ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kukuza Pato la Taifa.
Pia amesema watalii wanapotembelea kwa wingi wanatoa fursa kwa wananchi kwa kuuza bidhaa mbalimbali katika maeneo yanayozungukwa na hifadhi hivyo jamii inanufaika.
Alieleza kwamba wananchi tuendelee kutunza hifadhi zetu na maliasili ni za kwetu sote ili tuweze kupata fedha kwa ajili ya kuongeza ama kukuza uchumi ya nchi yetu.
Kwa upande wake, Afisa Habari TAWA ,Beatus Maganja amesema kwamba Serikali imeweka mazingira wezeshi kwa watanzania wote na wawekezaji kuwekeza .
Amesema kwamba wananchi watumie fursa ya maonesho kwenda kutembele na kujionea wanyama pori ambao wapo kabla ya kilele.
"Njooni watanzania kujionea wanyama kwani baadhi wanawaona wanyama katika kupitia luninga na kwenye mitandao ya kijamii lakini Leo hii ni fursa kuwaona wanyama pori kwa ukaribu zaidi na kwa uhuru",alisema Maganja
Hata hivyo amesema katika maonesho haya ni fursa mojawapo kwa wananchi kwani unaweza kuuliza maswali mbalimbali kuhusiana na tabia za wanyama wakali na waharibifu kwa mfano fisi madoa unaweza kujifinza tabia zao na kujua namna gani yakuweza kuepuka hawa wanyama katika maeneo mbalimbali waliokokua wakisumbua.
Naye Mlezi wa Kituo kulelea watoto wenye mahitaji maalum na wanaoishi katika mazingira magumu cha Wezesha Kupaa YWAM Mwandege,Rebecca amefurahia kutembelea Banda la TAWA kwa kujionea wanyama mbalimbali ambapo watoto wamejionea kwa macho na kwamba walikua wanasoma darasani kwa kuona kwenye picha. 

Comments
Post a Comment