JIMBO JIPYA LA KIVULE WAGOMBEA WAPISHANA .MAAMUZI YAPO KWA WAJUMBE.



Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline

                DAR ES SALAAM 

WAKATI zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa Watia Nia wa Ubunge, katika majimbo manne ya Wilaya ya Ilala, likihitimishwa, kwa Jumla ya Wagombea 84 Kati ya 87 waliochukua fomu hizo kuzirejesha.

 Hali ya joto la kinyang'anyiro hicho kwa wagombea katika Jimbo jipya la Kivule imezidi kuongezeka.

Kujitokeza kwa Komredi Brendan Maro, Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa na Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Tanzania (TUGHE) kunatajwa  kuongeza uganzi kwa watia nia wengine katika mchuano huo.

Komredi Maro, ambaye ni Mkazi wa Tawi la Kitundakati, Kata ya Kitunda, ni kada aliyelelewa ndani ya chama na hivyo kujipatia uzoefu was kiuongozi ndani na nje ya Chama cha Mapinduzi, ambako alianza kukitumikia akiwa Chipukizi wa chama cha Mapinduzi, huko wilayani Kilombero.

 Katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, Komredi Maro alikuwa mmoja wa Waratibu wa kundi la Vijana wa Vyuo Vikuu, wenye ushawishi waliotafuta Kura za ushindi wa kishindo kwa CCM, wakivuma kwa ljina la Wanamtandao.

Komredi Maro ambaye aliwahi kuhudumu pia kama Mratibu wa TUGHE Wilaya ya Ilala na Mwenyekiti wa Mkoa wa Shirikisho la Vyama huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) anakumbukwa kwa kujenga hoja na ushawishi mkubwa, wakati wa sakata la Sheria na Kanuni ya Mafao (Kikotoo), ambapo alifanikiwa kuwaunganisha Wafanyakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwashawishi kuwa watulivu kwa kuamini kwenye jitihada za majadiliano yanayoendelea baina ya Serikali na TUCTA, akiwa pia Mjumbe wa chombo kikuu cha maamuzi ndani ya Shirikisho hilo.

 Itakumbukwa hivi karibuni Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, kupitia maadhemisho ya Sherehe za Meimosi aliwatangazia Wafanyakazi na Wastaafu kuwa Serikali imepokea maoni ya wadau na imeelekeza kufanyika kwa marekebisho muhimu kwenye Kanuni ya kikotoo, huku pia akitangaza ongezeko la mishahara na ukomo wa kima cha chini cha mshahara wa serikali.

Komredi Maro, ambaye pia ni muhitimu wa Shahada ya Uzamili(MIB) kutoka Shule Kuu ya Uchumi na Biashara za Kimataifa ya Chuo Kikuu cha Uchumi na Fedha cha Jiangxi, katika Jimbo la Nanchang, nchini China, kwa sasa ni Afisa Mwandamizi wa Uhamasishaji Rasilimali na Usimamizi Miradi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania.

Komredi Maro anatajwa kuwa mmoja wa vijana makini mwenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo, kujenga hoja na kutoa kushawishi. Katika kuainisha ni zipi changamozo zinazolikabili Jimbo hilo jipya kwa sasa, 

Komredi Maro amejipambanua kwa uelewa mpana wa jiografia ya Jimbo hilo na amekuwa mtia nia pekee ambaye amekuwa akiainisha pia mikakati ya utatuzi wa changamoto zilizopo, huku akiipongeza Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa ujenzi na maboresho ya Hospitali ya Wilaya Kivule na Vituo vya utoaji huduma za afya jimboni humo, akisisitiza kuanza kwa kandarasi ya barabara ya Banana-Kitunda -Kivule-Msongola kutakuwa ni mkombozi wa maendeleo kwa Kata tatu zinazopitiwa na barabara hiyo, huku akiainisha mipango kamambe ya miradi ya kiuchumi kwa makundi ya Wanawake, Vijana, Wastaafu na Sekta Binafsi ndani ya Jimbo, katika kunufaika kimkakati na miundombinu hiyo.

Komredi Maro aliwasili katika Ofisi za CCM wilaya na kupokolewa na Chief Silvestry Yaredi, Katibu wa CCM wiyala ya Ilala, ambapo alikabidhi fomu zake majira ya Saa 7:05mchana na kuondoka.   



Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025