WAZIRI MKUU KUWA MGENI RAsMI KWENYE UZINDUZI WA "SAMIA LEGAL AID",
Na Angelina Mganga,DmNewsonline
DAR ES SALAAM
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majali anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kampeni ya msaada wa Kisheria ya Mama Samia itakayofanyika katika Viwanja vya Maturubai Mbagala Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Juni 13,2025 Jijini Dar es Salaam Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,Albert Chalamila amesema kutokana na changamoto mbalimbali za kisheria zinazowakabili wananchi hasa wa mkoa wa Dar es salaam,Wizara ya Katiba na Sheria kupitia kampeni hiyo itaendesha zoezi la kutoa msaada wa kisheria kwa siku 10 mfululizo kuanzia Juni 16-25,2025
RC Chalamila ametoa wito kwa wakazi wa Jiji hilo kuwa kampeni hii itazinduliwa siku hiyo na baada ya hapo itaendelea katika Halmashauri zote ndani ya mkoa huu
Ametaja huduma zitakazotolewa zinahusu msaada wa kisheria zikiwemo Mirathi,Migogoro ya adhi, uvunjifu wa haki na amani pamoja na nyingine zitatolewa na wataalamu wa masuala ya Sheria.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria .Ester Msambazi amesema kutokana na changamoto zilizopo katika Jamii kuhusu uelewa wa masuala ya kisheria,Serikali iliamua kuanzisha kampeni hiyo ya "Mama Samia Legal Aid" ili kuwsaidia wale ambao hawana uwezo wa kupata huduma hizo.
Kampeni hii itakuwa na msaada mkubwa kwa Wananchi ambao wengi wao wanashindwa kupata huduma za kisheria kutokana na kipato pamoja na kutokuwa na uelewa juu ya masuala ya kisheria 

Comments
Post a Comment