HALMASHAURI YA JIJI LA DAR YATENGA BILIONI 6.2 BAKETI YA 2025/2026 IDARA Y ELIMU SEKONDARI

Na Angelina Mganga,DmNewsOnline 
      ‎DAR ES SALAAM 
‎HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam wameketi katika kikao  kazi cha kutathimini miradi ya maendeleo ya Elimu Sekondari  ambapo mwaka 2025/2026 wametenga bilioni 6.2 kwenye bajeti katika ujenzi na uboredhaji wa miundo mbinu ndani ya Halmashauri.
‎Akizungumza katika kikao Leo Juni 12,2025  Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Jiji ,Elihuruma Mabelya amesema kwamba kikao hicho cha tathimini kinahusisha idara ya Elimu Sekondari ambapo tathimini hiyo imejikita katika kuhakikisha kwamba mapungufu ambayo yamejitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ndani ya mwaka wa fedha huu hayajitokezi mwaka wa fedha ujao.
‎"Tumejikita katika utekelezaji wa mwanzo mpya wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya elimu Sekondari",amesema
‎Amesema tumeshuhudia Idara ya elimu Sekondari imefanya vizuri kwenye michezo ya Umiseta ambapo wefanikiwa kupata vikombe vyakutosha na kuvikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo kwa heshima ya uongozi wake madhubuti ndani ya wilaya yetu.
‎Pia amemshukuru Mkuu wa wilaya huyo kwa kazi kubwa ya hamasa na tumepata mafanikio makubwa kwa utekelezaji wa miradi na mipango mizuri chini ya usimamizi wake .
‎"Tumepokea vifaa vya kisasa vyakiteknolojia smart screen ambazo zitatumikq katika ufundishaji wa masomo ndani ya shule za Sekondari na pia ipo shule ya mfano ndani ya Jiji la Dar es Salaam ambayo ni shule ya Kitunda Relini ni shule ambayo itakuwa na maabara ya kisasa ya sayansi na tayari shule ipo katika hatua nzuri ya ujenzi na smart  screen zitatumika kwa wanafunzi wa shule hiyo ili watoto wapate elimu Bora", amesema Mkurugenzi Elihuruma Mabelya
‎Hata hivyo, amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa uwezeshaji mkubwa katika idara ya elimu Sekondari kwani baadhi ya shule zinajengwa kwa mapato ya ndani  ambazo ni Ukonga Sekondari,Kipunguni,Bonyokwa na Kitunda Relini  ni mwongozo wa kibajeti ambapo ni maelekezo ya Rais Dkt.Samia
‎Aliendelea kushukuru Baraza la madiwani kwani ndio msingi muhimu wa maendeleo tuliyoyapata katika kata zote 36 mitaa 159  kwa usimamizi mzuri wa Baraza la madiwani na kamati zake kuhakikisha kwamba miradi inatimia kwa wakati na kuwanufaisha wananchi wa maeneo husika.
‎Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema kwamba walipatiwa na serikali bilioni 36 kwa eneo ya elimu Sekondari ila zilijitokeza changamoto kwa shule ya Kipunguni,Bonyokwa na Mnazi mmoja hazikukamilika kwa wakati lakini  Kwa Sasa shule 8 za ghorofa zinakwenda kukamilika pamoja na madarasa.
‎Katika bajeji ya 2025/2026 ambapo bajeti yake ni bilioni 6.2 hii itafanya miradi ya elimu Sekondari kukamilika kwa wakati.
‎Amemshukuru Mkurugenzi ,Sfisa elimu Sekondari,Walimu na wanafunzi walikwenda kwenye michezo ngazi ya mkoa kwa kuibuka washindi wa jumla  kwamba katika mashindano ya  umiseta Wilaya yetu imeibuka kidedea kwa elimu sekondari   kwa kujinyakulia vikombe ikiwa ni jitihada kwa watoto wetu kwa ngazi ya Sekondari na msingi.
‎Naye Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dr.Mussa Ally amewashukuru Mkurugenzi ,Mkuu wa Wilaya na katibu tawala wa wilaya ya Ilala kwa usimamizi wa viongozi hawa tumepata vikombe vingi na fedha nyingi za miradi lakini pia kupata vifaa vya kisasa vitakavyowezesha ufundishaji wetu ,hii ni dhamira njema ya viongozi katika kuwekeza katika sekta ya Elimu Sekondari ambayo watanzania wengi wanategemea kupata elimu iliyo Bora.
‎Ameongeza kwa kuwashukuru  walimu wot hasa Maafisa elimiu Kata,Wakuu wa shule,walimu wote walioshiriki kuleta mafanikio haya Idara ya elimu Sekondari ambapo inafanya tathimini yake.
‎Ameendelea kwa kusema  katika michezo wamepata makombe zaidi ya 18 walimu 10 kwenda kwenye michezo ya Umiseta Taifa ,vijana 55 kati ya 120 watashiriki Umiseta Taifa kwahiyo tunaamini kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam itaendelea kufanya vizuri zaidi katika nyanja zote. 


Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025