CCM YAWAONYA WATIA NIA WANAOTUMIA LUGHA ZA KASHFA.
Na Eliasa Ally DmnewsOline IRINGA
CHAMA cha Mapinduzi
mkoa wa Iringa kimetoa onyo kwa baadhi ya watia nia nafasi ya udiwani na ubunge Mkoani hapo ambao wamekuwa wakitumia lugha ya zihaka na kashfa kwa washindani wao ili kujenga ushawishi wa kuchaguliwa katika uchaguzi Mkuu ujao wa Octoba 2025.
Rai hiyo imetolewa leo hii Juni 16, 2025 na mjumbe wa kamati kuu ya CCM Taifa MCC Salim Abri Asas wakati akizingumza na wanahabari katika ofisi za chama hicho.
MCC amesema wapo baadhi ya watia Nia wa uongozi wanaita vyombo vya habari na kuanza kumsemea, kumkashifu na kumdhihaki diwani au mbunge aliye madarakani kwa kuyaanika madhaifu yake ili kujijengea ushawishi na imani ya kwa wanaomchagua akifafanua kuwa kufanya hivyo hakuna Tija na kunachafua Chama hicho.
Akifafanua zaidi hoja hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa Daud Yassin amewaonya hata wale wapambe wa viongozi hao wanaotoka lugha za zihaka akisema lugha hizo zitawaathiri viongozi wao wanaowanadi.
Comments
Post a Comment