ASASI YA KIRAIA YAAZIMISHA SIKU YA MAZINGIRA KWA KUFANYA USAFI FUKWE YA BAHARI YA HINDI
KATIBU wa Asasi ya kiraia ya Sustainable alliance Tanzania Paul Matonya amesema , Asasi hiyo ya kiraia inayoongozwa na vijana waliomaliza Vyuo vikuu hapa Nchini shughuli zake kubwa ni kuwezesha vijana na kuhusisha kwenye mambo mazima ya kupambana na Kuhamasisha kuleta afya Bora ya bahari .
Amesema yeye kama kiongozi na Mwanasayansi kwa upande wa bahari na katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani amewaongoza vijana wezake kufanya usafi wa Mazingira katika eneo la fukwe ya bahari ya hindi jijini Dar es salaam.
Akizungumza na Waandishi wa habari katika eneo la fukwe bahari Salenda mara baada ya kufanya usafi huo wa Mazingira ya bahari.Matonya amesema lengo la kufanya usafi sio kwa ajili ya kusafisha bahari pekee lakini pia wanajulisha ulimwengu au umma nini ambacho kinakuwa kinatokea kwenye fukwe ya bahari.
"Siku hii ya leo tunaitumia kufanya usafi na kukusanya taka zote zikiwemo za plastiki ambazo haziozi na zaidi zinakuwa katika Mazingira ya bahari hivyo leo hii tunazikusanya na baada ya hapa tunakuja na takwimu ambazo zitaeleza kwa kiasi gani hizi takataka zipo katika fukwe zetu kuzunguka Jiji la Dar es salaam "amesema
Kikubwa zaidi kuaambia umma kwamba namna gani hizi taka za plastiki zinakuwa na madhara makubwa sana kwenye Mazingira yenyewe,na watu lakini pia muhimu zaidi kwenye viumbe ambavyo vinakuwa vinapatikana baharini kwahiyo kikubwa leo kama mnavyoona tumeshafanya usafi kupitia vijana hawa zaidi ya 100 ambao tumeshiriki wote na wenyewe wametoka kwenye Asasi mbalimbali za kiraia ."amesitiza Matonya
Matonya ameongeza kuwa Kuna Asasi mbalimbali ambazo zinaongoza vijana kwa hapa Dar es salaam wakishirikiana kwa pamoja katika kufanya usafi huo nakwamba pia Kuna wanafunzi mbalimbali kutoka Vyuo vikuu wamejumuika hapa.
Akizungumzia taka hizo amefafanua kuwa baada ya kuzikusanya zinawafanya kupata takwimu ili kuweza kujua aina Gani ya taka ambazo zinachafua zaidi fukwe za bahari yetu na katika kuchambua wameona kuwa Kuna vitu mbalimbali kama Sindano za hospitalini ,taka za plastiki, chupa za maji , viatu pamoja na taka zingine za majumbani hivyo Chanzo kikubwa za hizo taka ni watu wenyewe
"Hapa sasa nitoe wito kwa watu wote kubadilika tabia kwa maana kwakufanya hivo kutafanya Kudhibiti hiki ambacho kinaonekana hapa leo ."amesema Matonya
Kwaupande wake Nasra Nurdin ambaye pia ni kiongozi kutoka Soa Tanzania amesema wametumia siku hiyo kuhamasishana kwa kufanya usafi katika eneo la Salenda ambapo pia imekwenda sambamba na siku ya Grobal ocean up ya mwaka 2025 na walikuja na vijana ili kuweza Kuhamasisha Kwa namna gani watafanya usafi kando ya bahari na kusaidia viumbe hai waliobaharini.
Amesema wameweza kufanya usafi kwa uwezo wao lakini huwezi kumaliza kufanya usafi wote kwa mara Moja hivyo wanahamasisha vijana wengine na jamii kujenga utaratibu wa kufanya usafi kando ya bahari ili kusaidia viumbe bahari kwani mwisho wa siku taka zote zinaishia huko na kupelekea athari kubwa kwa viumbe hao.
Nasra ameongeza kuwa Moja ya athari ambayo inapatikana baharini hususani kwa mnyama aina ya kasa ambao ni Moja ya viumbe ambao wanapatikana na mazingira yao ya kuzaliana yanakuwa ni kando ya bahari hivyo Mazingira yanapoharibiwa kando ya bahari yanapunguza mazaria ya kasa lakini pia plastiki zina athari kubwa kwasababu kasa anaweza kumeza plastic na kushindwa kuitoa na kuleta athari ya kifo chake na plastiki inatabia ya kujivunja na kutengeneza plastiki ndogo ndogo kitaalamu ni Micro _plastiki ambayo inakwenda kutoa athari ya uzalishaji wa viumbe hao.
Ameongeza kuwa athari nyingine ambayo inaweza kupatikana kwa viumbe hao ni uvuvi haramu hasa kwa kutumia nyavu kwani watu wanataka samaki na wakimvua kasa mara nyingi wanamrudisha kwenye maji wakati mungine akiwa ameshakufa hivyo wadau wa Mazingira waendelee kujitokeza kutoa elimu na kufanya usafi ili kupunguza tatizo kwa viumbe wa majini.
Naye Brenda Mollel kutoka taasisi ya vijana ya uhandisi amesema kutokana na changamoto za uchafunzi wa fukwe kando ya bahari wameamua kuungana ili kuweza kufanya usafi kwa lengo la kulinda Mazingira
Amesema kuwa fukwe nyingi kando ya bahari ni chafu sana na kwamba hata watu wanaozunguka kwenye fukwe hizo wanaufahamu mdogo kiasi kwamba wanashindwa hata kuhamasishana ili kufanya usafi kwenye Mazingira yanayowazunguka hivyo nakuwataka kuwa na hamasa ya kujitolea na kufanya usafi na si kusubiri kusukumwa
Lameck Joseph ambaye ni Mdau wa bahari amesema wamelazimika kufanya usafi katika fukwe za bahari ya Hindi eneo la Salenda ili kuweka usafi wa Mazingira nakwamba eneo hilo limeonekana kuathiriwa kwa kiasi kikubwa na taka zinazotoka kwenye Mazingira yetu majumbani
Amesema changamoto ya uchafunzi huo wa Mazingira ni kutokana na shughuli zetu wenyewe za Kila siku kwani Kila kitu kinachofanyika kinaathiri Mazingira kwa kiasi kikubwa na ndio maana Mazingira ya fukwe yamekua ya kiathiriwa na taka za aina tofauti.
Lameck amefafanua kuwa lazima Kila mtu awe na fikra za kutuza Mazingira yake ,kulinda Mazingira ili na yenyewe yaweze kumlinda kwasababu kubwa ya habari kwa upande wa bara inaathiriwa na taka zinazotokana na shughuli za mwanandamu kwahiyo kwa ujumla utatuzi unaaza kwa mtu binafsi kabla ya taasisi na zaidi kujua Umuhimu wa Mazingira yake ili aweze kuyatunza.
Comments
Post a Comment