Posts

Showing posts from May, 2025

POLISI DAR WATOA RAI KWA WATUMIAJI VYOMBO VYA MOTO KUFUATA SHERIA

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline                DAR ES SALAAM  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa rai kwa watumiaji wote wa barabara kuzingatia Sheria, Kanuni, na matumizi sahihi ya barabara muda wote wanapoendesha vyombo vya moto. Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 31,2025 Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalu ya Dar es Salaam,SACP Muliro Jumanne Muliro amesema mwezi Aprili hadi 31 Mei 2025 jumla ya madereva wa magari na pikipiki za maguruduamu matatu (Bajaj) wamekamatwa kwa kutumia barabara za mwendo kasi kinyume na sheria ni 289, pikipiki(bodaboda) 61, bajaj 65,magari ya Serikali 35, magari binafsi 123,walichukuliwa hatua kali za kisheria na wengine 41walionywa. Aidha ,amesema kwa kutumia kifungu Cha 45 na 46A vya Sheria ya Usalama barabarani sura ya 168 iliyorekebishwa mwaka 2002 kinachokataza dereva kutumia kilevi na kuendesha chombo Cha moto,ufuatiliaji maali usiku na mchana ulifanywa na kuwapima u...

VIJANA 26 KUSHIRIKI PROGRAMU YA MANDELA WASHINGTON FELLOSHIP2025 NCHINI MAREKANI

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                  DODOMA VIJANA  waliochaguliwa kushiriki progranu ya Mandela Washington Fellowship kwa mwaka 2025, wamekumbushwa kuwa fursa waliyoipata haikuja kwa bahati, isipokuwa kutokana na majukumu wanayoyafanya ambayo yana mchango mkubwa kwa jamii. Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa wakati anawapa nasaha za kuwaaga vijana hao 26 jijini Dodoma Mei 30, 2025. Balozi Mussa aliwataka kutumia fursa hiyo kujifunza mambo mapya kwa kuwa nchi wanayokwenda imeendelea kiuchumi na kiteknolojia duniani na itawapa fursa pia ya kukutana na raia wa mataifa mbalimbali wenye uzoefu na mila tofauti. Vijana hao ambao wanatarajiwa kwenda nchini Marekani Juni na kurejea Agosti 2025,  wametakiwa kulitangaza jina la Tanzania kwa watu watakaokutana nao.  "Mtalitangaza jina la nchi yetu kwa kuheshimu sheria za nchi mnayokwenda, ...

Vijana 26 Kushiriki progranu ya Mandela Washington Fellowship 2025 nchini Marekani

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline Dodoma Vijana waliochaguliwa kushiriki progranu ya Mandela Washington Fellowship kwa mwaka 2025, wamekumbushwa kuwa fursa waliyoipata haikuja kwa bahati, isipokuwa kutokana na majukumu wanayoyafanya ambayo yana mchango mkubwa kwa jamii. Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa wakati anawapa nasaha za kuwaaga vijana hao 26 jijini Dodoma Mei 30, 2025. Balozi Mussa aliwataka kutumia fursa hiyo kujifunza mambo mapya kwa kuwa nchi wanayokwenda imeendelea kiuchumi na kiteknolojia duniani na itawapa fursa pia ya kukutana na raia wa mataifa mbalimbali wenye uzoefu na mila tofauti. Vijana hao ambao wanatarajiwa kwenda nchini Marekani Juni na kurejea Agosti 2025,  wametakiwa kulitangaza jina la Tanzania kwa watu watakaokutana nao. "Mtalitangaza jina la nchi yetu kwa kuheshimu sheria za nchi mnayokwenda,  kutangaza utamaduni mzuri wa Tanzania na kuelezea kwa ufasaha mambo makub...

ABSA DAR CITY MARATHON YAKABIDHI VIFAA TIBA KWA WANAWAKE WAJAWAZITO NA WATOTO HOSPITALI YA MNAZI MMOJA

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline Dar Es Salaam. Katika kuimarisha Huduma za Afya ya Uzazi nchini Klabu ya Riadha ya 'The Runners, imetoa vifaa tiba kwa wanawake wajawazito na watoto wachanga katika Hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam. Vifaa hivyo ni kipimajoto cha kidigitali, seti za sindano maalum (cannulas), na kifaa cha kufuatilia afya ya mtoto tumboni (fetal monitor) Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa hafla ya makabidhiano, msemaji wa klabu hiyo, Godphrey Mindu, amesema kuwa vifaa hivyo ni kwa ajili ya watoto walioko tumboni,waliotoka kuzaliwa pamoja na wanawake wajawazito. Ameongeza kuwa vifaa hivyo vimetolewa kama sehemu ya kuiunga mkono serikali na Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kuboresha huduma ya mama na mtoto na kuhakikisha usalama wa mama wajawazito na watoto wao Ametoa wito kwa wadau wengine kuungana na serikali kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya wengine. Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk L...

WAJUMBE WA MKUTANO MKUU CCM WAKIBURUDIKA KUELEKEA KUZINDUA ILANI

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsonline                DODOMA WAJUMBE  wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiburudika burudani ya mziki kutoka Kikundi cha Sanaa cha Tanzania One Theatre (TOT), kikiongozwa na Malkia wa Mipasho na Mziki wa Taarab, Bi. Khadija Omar Abdallah Kopa, leo Ijumaa tarehe 30 Mei 2025, jijini Dodoma.  Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Taifa huo ukiongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ulianza jana Alhamis, tarehe 29 Mei 2025, na leo unaendelea katika siku yake ya pili, katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma, ambapo mojawapo ya agenda itakuwa ni kuzindua Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2025 - 2030.  

DKT MPANGO ATETA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE ,DENNIS LONDO

Image
Na Mwandishi Wetu,DmNewsonline  MAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dennis Londo, Balozi wa Tanzania nchini Ivory Coast mwenye Makazi yake nchini Nigeria Balozi Selestine Kakele,  Mungine ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Juma Malik Akil kando ya Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaofanyika katika Hoteli ya Sofitel Ivoire Jijini Abidjan nchini Ivory Coast.

TAKUKURU TABORA YANASA WEZI WA MALI ZA WAKULIMA

Image
           Na Allan Kitwe,DmNewsonline                     TABORA  TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Tabora imenasa jumla ya wafanyabiashara 7 waliokuwa wakiuza mali za wizi za wakulima wa zao la tumbaku zenye thamani ya sh bil 1.4. Mkuu wa TAKUKURU Mkoani hapa Azza Mtaita amethibitisha kukamatwa watuhumiwa hao alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake jana na kueleza kuwa wafanyabiashara hao wamekamatwa katika operesheni maalumu. Amebainisha mali zilizokamatwa kuwa ni mabelo ya magunia ya kufungashia zao hilo yajulikanayo kama majafafa ambayo ni mali halali ya wakulima, jumla ya magunia 2,681 yenye thamani ya sh bil 1.4 yamekamatwa katika maeneo tofauti. Kamanda Mtaita amefafanua kuwa magunia hayo yamekamatwa kutoka kwa wafanyabiashara baada ya kukutwa wakiyauza kinyume na taratibu huku wakijua fika kuwa ni mali halali ya wakulima kwa sababu waliyanunua msimu uli...

TANZANIA NA JAPAN ZATIA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

Image
Na Mwandishi wetu,DmNewsOnline               TOKYO JAPAN SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan zimetia saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika mpango wa pamoja wa uwekezaji katika Biashara ya Kaboni utakaowezesha kampuni za nchi hizo mbili kuwekeza katika Biashara ya Kaboni nchini Tanzania. Utiaji saini wa makubaliano hayo umefanyika Mei 28, 2025  Tokyo, Japan kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni na Serikali ya Japan ikiongozwa na Waziri wa Mazingira, Mhe. Asao Keiichiro (Kei). Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo, Waziri Masauni amesema Makubaliano ya Mashirikiano yaliyosainiwa yamekusudiwa kuimarisha uhusiano kati ya Japan na Tanzania kwa maendeleo endelevu na hatua za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. . Go to the bow bow. Amesema mashirikano haya yataongeza  fursa ya ...