VIONGOZI NA WANANCHI TUSHIRIKIANE UJENZI UWANJA WA MPIRA ILI KWENDA KWA KASI INAYOTAKIWA.PROF.KABUDI

Na Deborah Lemmubi,DmNewsonline

                 DODOMA

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi ametoa Rai kwa Viongozi na Wananchi wa Jiji la Dodoma kushirikiana kwa karibu katika kusimamia mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa Kisasa ikiwemo kukamilisha miundombinu wezeshi itakayomsaidia Mkandarasi kwenda kwa kasi inayotakiwa katika ujenzi wa uwanja.

Prof.Kabudi amesema haya wakati wa hafla ya utiaji saini Mkataba wa Ujenzi wa uwanja wa mpira Dodoma sambamba na kumkabidhi kazi Mkandarasi katika hafla iliyofanyika leo Februari 13,2025 jijini Dodoma .

Amesema moja kati ya vitu muhimu ambavyo vinapaswa kuwepo wakati wa utekelezaji wa ujenzi huo ni pamoja na kupataikana kwa Maji,Umeme, Huduma za zima moto na Mazingira wezeshi ya kuweza kufika katika eneo hilo kunakojengwa uwanja huo.

"Ndugu viongozi na ndugu wananchi katika kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati ni dhahiri kwamba lazima tushirikiane kwa karibu katika kusimamia mradi huu sambamba na kukamilisha miundombinu wezeshi itakayomrahisishia Mkandarasi kwenda kwa kasi inayotakiwa, na baadhi ya masuala muhimu ni pamoja na kupatikana kwa vifaa vyote muhimu ikiwemo maji,umeme, huduma ya zimamoto na mazingira rafiki ya kufika kwa haraka katika ebeo la mradi".

Akizungumza katika Mradi huo amesema uwanja huu utakapokamilika utakuwa ni moja kati ya alama za kudumu zinazoutambulisha Mkoa wa Dodoma kwakuwa zamani Mkoa huo ulitambulika kwa alama kama kanisa la roho mtakatifu maarufu kwa jina la mtungi,Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ikaongezeka Jengo la Mahakama lakini sasa  alama nyingine ambayo ni uwanja wa mpira unaojengwa katika eneo changamano la michezo Dodoma.

Sambamba na hayo Prof. Kabudi amewahamasisha wana Dodoma kuchangamkia fursa zitakazo jitokeza katika ujenzi wa uwanja huo ili kuongeza kipato kwani kutakuwako na fursa ikiwemo biashara na kazi mbalimbali wakati ujenzi huo ukiendelea.

Akitoa salamu kwa niaba ya wana Dodoma Mbunge wa Dodoma Mjini na Waziri wa Madini Mhe Anthony Mavunde amesema ujenzi wa uwanja unatumia asilimia 100 ya fedha za Serikali lakini pia ni moja kati ya maamuzi magumu ya  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwepo kwa kusua sua kwa muda mredu juu ya ujenzi wa uwanja huo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Rosemary Senyamule unaongoza kuwa Mkoa wa Dodoma una vipaumbele vingi lakini moja wapo ni Utalii na utalii huo ni pamoja kuwa na utalii wa michezo

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge  Elimu utamaduni na Michezo Husna Sekiboko amesema kuwa shahuku yao ni kuona ujenzi huo wa uwanja wa mpira unazingatia muda  kwa maana ya kukamilika kwa wakati na kuendana sawa na thamani ya pesa iliyowekezwa kutumika katika kujenga uwanja huo.

Uwanja huu utakapokamilika unatarajia kuchukua watu elfu 32 ma utajengwa ndani ya miezi 24.

Comments

Popular posts from this blog

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE TAMISEMI YAKOSHWA NA UBORA WA MIRADI YA MAENDELEO KIBAHA TC

MAMBO 10 MAZITO YANAYOIANGAMIZA NA KUIZAMISHA CHADEMA 2024/2025